0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

99. MLANGO WA MAPENDEKEZO YA KUUTANGULIZA UPANDE WA KULIA KATIKA KILA JAMBO LA KHERI

– باب استحباب تقديم اليمين في كل مَا هو من باب التكريم


كالوضوءِ وَالغُسْلِ وَالتَّيَمُّمِ، وَلُبْسِ الثَّوْبِ وَالنَّعْلِ وَالخُفِّ وَالسَّرَاوِيلِ وَدُخولِ الْمَسْجِدِ، وَالسِّوَاكِ، وَالاكْتِحَالِ، وَتقليم الأظْفار، وَقَصِّ الشَّارِبِ، وَنَتْفِ الإبْطِ، وَحلقِ الرَّأسِ، وَالسّلامِ مِنَ الصَّلاَةِ، وَالأكْلِ، والشُّربِ، وَالمُصافحَةِ، وَاسْتِلاَمِ الحَجَرِ الأَسْوَدِ، والخروجِ منَ الخلاءِ، والأخذ والعطاء وغيرِ ذَلِكَ مِمَّا هُوَ في معناه. ويُسْتَحَبُّ تَقديمُ اليسارِ في ضدِ ذَلِكَ، كالامْتِخَاطِ وَالبُصَاقِ عن اليسار، ودخولِ الخَلاءِ، والخروج من المَسْجِدِ، وخَلْعِ الخُفِّ والنَّعْلِ والسراويلِ والثوبِ، والاسْتِنْجَاءِ وفِعلِ المُسْتَقْذرَاتِ وأشْبَاه ذَلِكَ

قَالَ الله تَعَالَى: ﴿فَأَمَّا مَنْ أوتِيَ كِتَابَهُ بيَمينِهِ فَيْقُولُ هَاؤُمُ اقْرَأوا كِتَابِيْه﴾ [ الحاقة: 19 ] الآيات

وقَالَ تَعَالَى: ﴿فَأصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ مَا أصْحَابُ المَيْمَنَةِ وَأَصْحابُ المَشْئَمَةِ مَا أصْحَابُ المَشْئَمَةِ﴾ [ الواقعة: 8-9 ]


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



99. MLANGO: SUNNAH YA KUUTANGULIZA UPANDE WA KULIA KATIKA KILA JAMBO LA KHERI KAMA VILE KUTAWADHA, KUOGA, KUTAYAMAMU, KUVAA NGUO, VIATU, KHUFFU NA KUVAA SURUALI, KUINGIA MSIKITINI, KUPIGA MSWAKI, KUPAKA WANJA, KUKATA KUCHA, KUPUNGUZA MASHARUBU, KUSUMUA NYWELE ZA MAKWAPA, KUNYOA KICHWA, KUTOA SALAMU KATIKA SWALA, KULA, KUNYWA, KUPEANA MIKONO, KULIINULIA MKONO JIWE LEUSI, KUTOKA CHOONI, KUCHUKUA, KUPOKEA NA MENGINEYO YALIOMO KATIKA HAYO. NA YAPENDEKEZWA KUUTANGULIZA UPANDE WA KUSHOTO KATIKA KINYUME CHA MAMBO HAYO KAMA VILE KUTEMA KOHOZI NA MATE, KUINGIA CHOONI, KUTOKA MSIKITINI, KUVUA KHUFFU, VIATU, SURUALI NA NGUO, KUTAMBA, KUTENDA MATENDO YANAYOFUNGAMANA NA TAKA NA MFANO WAKE


Mwenyezi Mungu Amesema: “Basi yule atakayepewa daftari lake kwa mkono wake wa kuume (kulia) atasema (kwa furaha): “Haya! Someni daftari langu (nililopewa sasa hivi).” Mpaka mwisho wa Aya zinazoeleza habari hii. [69:19].

Mwenyezi Mungu Allâh Amesema: “Watu wenye kheri (walio upande wa kulia); watakuwa namna gani hawa watu wenye kheri! Na watu wenye shari (walio upande wa kushoto); watakuwa namna gani hawa watu wenye shari!” [56:8, 9].

Begin typing your search above and press return to search.