0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

717. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Kuomba istikhara na Kutaka ushauri

باب الاستِخارة والمشاورة


وعن جابر – رضي الله عنه -، قَالَ: كَانَ رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم – يُعَلِّمُنَا الاسْتِخَارَةَ في الأمُورِ كُلِّهَا كَالسُّورَةِ مِنَ القُرْآنِ، يَقُولُ: {إِذَا هَمَّ أحَدُكُمْ بِالأمْرِ، فَلْيَركعْ ركْعَتَيْنِ مِنْ غَيْرِ الفَرِيضَةِ، ثُمَّ ليقل: اللَّهُمَّ إنِّي أسْتَخِيرُكَ بِعِلْمِكَ، وَأسْتَقْدِرُكَ بِقُدْرَتِكَ، وأسْألُكَ مِنْ فَضْلِكَ العَظِيْمِ، فَإنَّكَ تَقْدِرُ وَلاَ أقْدِرُ، وَتَعْلَمُ وَلاَ أعْلَمُ، وَأنْتَ عَلاَّمُ الْغُيُوبِ. اللَّهُمَّ إنْ كُنْتَ تَعْلَمُ أنَّ هَذَا الأمْرَ خَيْرٌ لِي في دِينِي وَمَعَاشِي وَعَاقِبَةِ أمْرِي} أَوْ قَالَ: {عَاجِلِ أمْرِي وَآجِلِهِ، فاقْدُرْهُ لي وَيَسِّرْهُ لِي، ثُمَّ بَارِكْ لِي فِيهِ. وَإنْ كُنْتَ تَعْلَمُ أنَّ هَذَا الأَمْرَ شَرٌّ لِي في دِينِي وَمَعَاشِي وَعَاقِبَةِ أَمْرِي} أَوْ قَالَ: {عَاجِلِ أمْرِي وَآجِلِهِ؛ فَاصْرِفْهُ عَنِّي، وَاصْرِفْنِي عَنْهُ، وَاقْدُرْ لِيَ الخَيْرَ حَيْثُ كَانَ، ثُمَّ أرْضِنِي بِهِ} قَالَ: {وَيُسَمِّيْ حَاجَتَهُ}    رواه البخاري


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa na Jâbir (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Mtume (ﷺ) alikuwa akitufundisha istikhâra katika mambo yote kama vile anavyotufundisha Sûra katika Qur’âni, akituambia: “Mmoja wenu anapoazimia kufanya jambo, aswali rakaa mbili ambazo si za faradhi, kisha aseme: Allâhumma innî astakhîruka bi‘ilmika wa astaqdiruka biqudratik, wa as-aluka min fadhlikal‘adhwîm, fa innaka taqdiru walâ aqdir, wa ta’lamu walâ a’lam, wa anta ‘allâmulghuyûb. Allâhumma in kunta ta’lamu anna hâdhal-amra khairullî fî dînî wa ma‘âshî wa ‘âqibati amrî.. [Ewe Mola, hakika mimi nakuomba ushauri kwa Ilimu Yako, nakuomba uwezo kwa Uwezo Wako na nakuomba fadhila Zako Kubwa. Ni hakika Wewe Ndiwe Unayeweza nami sina uwezo, Unajua, nami sijui, Nawe ni Mjuzi wa ghaibu. Ewe Mola, Wewe Ndiwe Unayejua iwapo jambo hili lina kheri kwangu katika Dini yangu, maishani mwangu na mwisho wa mambo yangu._” Au alisema: “‘âjili amrî wa âjilih, faqdurhu lî wayassirhu lî thumma bârik lî fîh, wa in kunta ta’lamu anna hâdhal amra sharrulli fî dînî wa ma‘âshî wa‘âqibati amrî.. […katika dunia yangu na Akhira yangu, basi Nikadirie, Unisahilishie kisha Unibarikie. Nawe Ndiwe Unayejua, ikiwa jambo hili lina shari kwangu katika Dini yangu, maishani mwangu na mwisho wa mambo yangu._” Au alisema:‘âjili amrî wa âjilih, fasrifhu ‘annî wasrifnî ‘anhu waqdurliyalkhaira haithu kâna thumma raddhinî bih.” ]..katika dunia yangu na Akhira yangu, basi Uniepushie jambo hilo, Uniepushe mimi na jambo hili na Unikadirie kheri popote inapokuwa, kisha Unijaalaie kuwa radhi._” Akasema: “Kisha aitaje haja yake.”   [ Imepokewa na Bukhârî.]

Begin typing your search above and press return to search.