0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

668. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Wajibu Wa Kuwatii Wenye Madaraka Katika Jambo Ambalo Si La Kumuasi Allah Na Uharamu Wa Kuwatii Katika Maasia

 باب وجوب طاعة ولاة الأمر في غير معصية وتحريم طاعتهم في المعصية


 وعن أَبي هُنَيْدَةَ وَائِلِ بن حُجرٍ – رضي الله عنه -، قَالَ: سَألَ سَلَمَةُ بن يَزيدَ الجُعفِيُّ رسولَ الله – صلى الله عليه وسلم -، فَقَالَ: يَا نَبِيَّ الله، أرأيتَ إنْ قامَت عَلَيْنَا أُمَرَاءُ يَسألُونَا حَقَّهُم، وَيمْنَعُونَا حَقَّنَا، فَمَا تَأْمُرُنَا؟ فَأعْرَضَ عنه، ثُمَّ سَألَهُ، فَقَالَ رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم -: { اسْمَعْوا وَأَطِيعُوا، فإنَّمَا عَلَيْهِمْ مَا حُمِّلُوا، وَعَلَيْكُمْ مَا حملْتُمْ}     رواه مسلم


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Abû Hunaidah, Wâ-il bin Hujri (Radhi za Allah ziwe juu yake ) amesema: “Salamah bin Yazîd al-Ju’fy alimwuliza Mtume (ﷺ): “Yâ Nabiyyallâh, nieleze lau viongozi watatusimamia wakituomba haki yao na wakitunyima haki yetu, watuamuru tufanye nini?” (Mtume) akajiepusha naye. Naye akamwuliza tena. Mtume (ﷺ) akamwambia: “Sikilizeni na mutii; hakika wao watapata dhambi kwa kutowajibika kwao nanyi mtapata dhambi kwa kuacha kusikia na kutii.”      [Imepokewa na Muslim.]

Begin typing your search above and press return to search.