0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

71. MLANGO WA KUWANYENYEKEA WAUMINI

باب التواضع وخفض الجناح للمؤمنين


قَالَ الله تَعَالَى: ﴿وَاخْفِضْ جَنَاحَكَ لِمَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ المُؤْمِنِينَ﴾ [ الشعراء: 215 ]

وقال تَعَالَى: ﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَنْ يَرْتَدَّ مِنْكُمْ عَنْ دِينهِ فَسَوْفَ يَأتِي اللهُ بِقَومٍ يُحِبُّهُم وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى المُؤْمِنينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الكَافِرِينَ﴾ [ المائدة: 54 ]

وقال تَعَالَى: ﴿يَا أَيُّهَا النَّاسُ إنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ ذَكَرٍ وَأُنْثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوباً وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللهِ أَتْقَاكُمْ﴾ [ الحجرات: 12 ]

وقال تَعَالَى: ﴿فَلاَ تُزَكُّوا أَنْفُسَكُمْ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اتَّقَى﴾ [ النجم: 32 ]

وقال تَعَالَى: ﴿وَنَادَى أَصْحَابُ الأَعْرَافِ رِجَالاً يَعْرِفُونَهُمْ بِسِيمَاهُمْ قَالُوا مَا أَغْنَى عنكم جَمْعُكُمْ وَمَا كُنْتُمْ تَسْتَكْبِرُونَ أَهؤُلاَءِ الَّذِينَ أَقْسَمْتُمْ لا يَنَالُهُمُ اللهُ بِرَحْمَةٍ ادْخُلُوا الجَنَّةَ لاَ خَوْفٌ عَلَيْكُمْ وَلاَ أَنْتُمْ تَحْزَنُونَ﴾ [ الأعراف: 48-49 ]


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى


 


71. MLANGO WA KUWANYENYEKEA WAUMINI


Mwenyezi Mungu Amesema: “: “Na uinamishe bawa lako kwa yule anayekufuata katika wale walioamini.”   [26:215].

Mwenyezi Mungu Amesema: “Enyi mlioamini! Atakayeiacha miongoni mwenu Dini yake, basi Allâh Atakujaleta watu Anaowapenda nao wanampenda, wanyenyekevu kwa Waumini na wenye nguvu juu ya makafiri..” [5:54].

Mwenyezi Mungu Amesema: “Enyi watu! Hakika Sisi Tumewaumba kutokana na mwanamume na mwanamke. Na Tumewajaalia kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Allâh ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi.” [49: 13].

Mwenyezi Mungu Amesema: “Basi msizitakase (msizisifu) nafsi zenu; Yeye Anamjua sana aliyetakasika (na asiyetakasika).”  [53:32].

Mwenyezi Mungu Amesema“Na hao watu wa al-A’râf, watawaita watu wanaowajua kwa alama zao. Watasema: Kujumuika kwenu hakukuwafalia kitu, wala hicho mlichokuwa mnafanyia kibri. Je, hawa sio wale mliokuwa mkiwaapia kuwa Allâh Hatawafikishia rehema. Ingieni Peponi, hapana khofu kwenu, wala hamtahuzunika!”   [7:48, 49].


Begin typing your search above and press return to search.