0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

566. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Kumtanguliza Mwenzio Na Kufarijian.

باب الإيثار والمواساة


وعن سهل بن سعدٍ – رضي الله عنه -: أنَّ أمْرَأةً جَاءَتْ إِلَى رسول الله – صلى الله عليه وسلم – بِبُرْدَةٍ مَنْسُوجَةٍ، فَقَالَتْ: نَسَجْتُها بِيَدَيَّ لأَكْسُوكَهَا، فَأَخَذَهَا النَّبيُّ – صلى الله عليه وسلم – مُحْتَاجاً إِلَيْهَا، فَخَرَجَ إِلَيْنَا وَإنَّهَا إزَارُهُ، فَقَالَ فُلانٌ: اكْسُنِيهَا مَا أحْسَنَهَا ! فَقَالَ: { نَعَمْ} فَجَلَسَ النَّبيُّ – صلى الله عليه وسلم – في المَجْلِسُ، ثُمَّ رَجَعَ فَطَواهَا، ثُمَّ أرْسَلَ بِهَا إِلَيْهِ: فَقَالَ لَهُ الْقَومُ: مَا أحْسَنْتَ ! لَبِسَهَا النَّبيُّ – صلى الله عليه وسلم – مُحتَاجَاً إِلَيْهَا، ثُمَّ سَألْتَهُ وَعَلِمْتَ أنَّهُ لا يَرُدُّ سَائِلاً، فَقَالَ: إنّي وَاللهِ مَا سَألْتُهُ لألْبِسَهَا، إنَّمَا سَألْتُهُ لِتَكُونَ كَفنِي. قَالَ سَهْلٌ: فَكَانَتْ كَفَنَهُ.      رواه البخاري


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Sahli bin Sa’d (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia kuwa, mwanamke mmoja alikuja kwa Mtume akiwa ana shuka iliofumwa, akamwambia Mtume : “Nimeifuma kwa mikono yangu ili nikuvishe.” Mtume akaichukua akiwa ana haja nayo, akaondoka mbele yetu akiwa ameifanya ni kikoi chake. Mtu mmoja akamwambia: “Nivalishe mimi, ni nzuri!” Akamwambia: “Sawa.” Mtume akaketi katika majilisi, kisha akarudi (nyumbani) akaikunja na akamtumia. Watu wakamlaumu: “Hukufanya vizuri! Mtume ameivaa akiwa ana haja nayo kisha ukamuomba, nawe wajua kuwa yeye hamnyimi muombaji!” Akasema: “Wallahi sikumuomba ili niivae, nimemwomba ili ipate kuwa ndio sanda yangu.” Sahli anaeleza: “Shuka hiyo ikawa ndio sanda yake.”   [ Imepokewa na Muslim.]

Begin typing your search above and press return to search.