0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

535. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Ukinaifu, Kujizuiya Kuomba Kufanya Iktisadi Katika Maisha….

باب القناعة والعَفاف والاقتصاد في المعيشة والإنفاق وذم السؤال من غير ضرورة


 وعن أَبي بِشْرٍ قَبيصَةَ بنِ المُخَارِقِ – رضي الله عنه -، قَالَ: تَحَمَّلْتُ حَمَالَةً فَأتَيْتُ رسولَ الله – صلى الله عليه وسلم – أسْأَلُهُ فِيهَا، فَقَالَ: { أقِمْ حَتَّى تَأتِيَنَا الصَّدَقَةُ فَنَأمُرَ لَكَ بِهَا} ثُمَّ قَالَ: { يَا قَبيصةُ، إنَّ المَسْأَلَةَ لاَ تَحِلُّ إِلاَّ لأَحَدِ ثلاثَةٍ: رَجُلٌ تحمَّلَ حَمَالَةً، فَحَلَّتْ لَهُ المَسْأَلَةُ حَتَّى يُصِيبَها، ثُمَّ يُمْسِكُ، وَرَجُلٌ أصَابَتْهُ جَائِحَةٌ اجْتَاحَتْ مَالَهُ، فَحَلَّتْ لَهُ الْمَسْأَلَةُ حَتَّى يُصِيبَ قواماً مِنْ عَيش – أَوْ قَالَ: سِدَاداً مِنْ عَيْشٍ – وَرَجُلٌ أصَابَتْهُ فَاقَةٌ، حَتَّى يَقُولَ ثَلاَثَةٌ مِنْ ذَوِي الحِجَى مِنْ قَوْمِه: لَقَدْ أصَابَتْ فُلاناً فَاقَةٌ. فَحلَّتْ لَهُ الْمَسْأَلَةُ حَتَّى يصيب قواماً من عيش، أَوْ قَالَ: سداداً من عيشِ، فما سِوَاهُنَّ مِنَ المسألَةِ يَا قَبِيصَةُ سُحْتٌ، يَأكُلُهَا صَاحِبُهَا سُحْتاً}     رواه مسلم.


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Abû Bishri, Qabîsa bin al-Mukhâriq (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Nilijitwika dhamana (ya kusuluhisha baina ya makundi mawili yaliozozana), nikamwendea Mtume nikimuomba dhamana hiyo. Akaniambia: “Subiri mpaka tuletewe sadaka halafu tutaamuru upewe.” Kisha akanambia: “Ee Qabîsa, hakika kuomba si halali kwa yeyote ila kwa watu watatu: mtu aliechukua dhamana (ya kusuluhisha baina ya makundi mawili yaliozozana), hapo ni halali kwake kuomba mpaka aipate, kisha atajizuwia, mtu aliefikiwa na gharika (au maafa makubwa) iliyoangamiza mali yake, hapo ni halali kwake kuomba mpaka apate kitakachomsaidia maishani mwake, na mtu aliepatwa na uhitaji, mpaka watu watatu wenye busara katika jamaa zake waseme “hakika fulani amepatwa na uhitaji!” hapo ni halali kwake kuomba mpaka atakapopata kitakachomsaidia maishani mwake. Kuomba kusikotokana na sababu hizo, ni haramu ee Qabisa, anayekula anakula haramu.”   [ Imepokewa na Muslim.]

Begin typing your search above and press return to search.