0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

523. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Ukinaifu, Kujizuiyz Kuomba Kufanya Iktisadi Katika Maisha….

باب القناعة والعَفاف والاقتصاد في المعيشة والإنفاق وذم السؤال من غير ضرورة


وعن حكيم بن حزام – رضي الله عنه -، قَالَ: سألتُ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – فَأعْطَانِي، ثُمَّ سَألْتُهُ فَأَعْطَانِي، ثُمَّ سَألْتُهُ فَأعْطَانِي، ثُمَّ قَالَ: { يَا حَكِيم، إنَّ هَذَا المَالَ خَضِرٌ حُلْوٌ، فَمَنْ أخَذَهُ بِسَخَاوَةِ نَفسٍ بُورِكَ لَهُ فِيهِ، وَمَنْ أخَذَهُ بإشرافِ نَفسٍ لَمْ يُبَارَكْ لَهُ فِيهِ، وَكَانَ كَالَّذِي يَأكُلُ وَلاَ يَشْبَعُ، وَاليَدُ الْعُلْيَا خَيْرٌ مِنَ اليَدِ السُّفْلَى} قَالَ حكيم: فقلتُ: يَا رسول الله، وَالَّذِي بَعَثَكَ بِالحَقِّ لاَ أرْزَأُ أحَداً بَعْدَكَ شَيْئاً حَتَّى أُفَارِقَ الدُّنْيَا، فَكَانَ أَبُو بَكْرٍ – رضي الله عنه – يَدْعُو حَكيماً لِيُعْطِيَه العَطَاء، فَيَأبَى أنْ يَقْبَلَ مِنْهُ شَيْئاً، ثُمَّ إنَّ عُمَرَ – رضي الله عنه – دَعَاهُ لِيُعْطِيَه فَأَبَى أنْ يَقْبَلَهُ. فقالَ: يَا مَعْشَرَ المُسْلِمِينَ، أُشْهِدُكُمْ عَلَى حَكيمٍ أنّي أعْرِضُ عَلَيْهِ حَقَّهُ الَّذِي قَسَمَهُ اللهُ لَهُ في هَذَا الفَيء فَيَأبَى أنْ يَأخُذَهُ. فَلَمْ يَرْزَأْ حَكيمٌ أحَداً مِنَ النَّاسِ بَعْدَ النبي – صلى الله عليه وسلم – حَتَّى تُوُفِّي.   متفقٌ عَلَيْهِ


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Hakîm bin Hizâm (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Nilimuomba Mtume ﷺ akanipa, kisha nikamuomba, akanipa, kisha nikamuomba akanipa, halafu akaniambia: “Ee Hakîm, hii mali ni rangi ya kijani (inapendeza) na ni tamu, anayeichukua kwa ukwasi wa moyo atabarikiwa, na anayeichukua kwa tamaa ya nafsi hatabarikiwa, na atakuwa ni kama yule anayekula wala hashibi, mkono ulio juu ni bora kuliko mkono ulio chini.” Nikasema: “Yâ Rasûlallâh, naapa kwa Aliekutumiliza kwa haki! Sitachukua chochote kutoka kwa yeyote baada yako mpaka niondoke duniani.” Abûbakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) akawa akimwita Hakîm ili ampe (haki yake) akawa anakataa kukubali kitu kutoka kwake. Kisha ‘Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) alimwita ili ampe, akakataa kupokea. ‘Umar akasema: “Enyi Waislamu, nawashuhudilia juu ya Hakîm kuwa mimi nampa haki yake ambayo Allâh Amemgawia katika ghanima hii naye anakataa kuichukua.” [Mpokezi aeleza:_ “Basi Hakîm hakuchukua chochote kutoka kwa yeyote baada ya Mtume ﷺ mpaka akafariki.”  [ Wameafikiana Bukhari na Muslim]

Begin typing your search above and press return to search.