0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

491. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Fadhila Ya Njaa, Maisha Ya Chini Kutosheka Kwa Vichache Katika Vyakula…..

 باب فضل الجوع وخشونة العيش والاقتصار عَلَى القليل من المأكول والمشروب والملبوس وغيرها من حظوظ النفس وترك الشهوات


وعن عروة، عن عائشة – رضي الله عنها -، أنّها كَانَتْ تقول: وَاللهِ، يَا ابْنَ أُخْتِي، إنْ كُنَّا نَنْظُرُ إِلَى الهِلاَلِ، ثُمَّ الهِلالِ: ثَلاَثَةُ أهلَّةٍ في شَهْرَيْنِ، وَمَا أُوقِدَ في أبْيَاتِ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – نَارٌ. قُلْتُ: يَا خَالَةُ، فَمَا كَانَ يُعِيشُكُمْ؟ قالت: الأَسْوَدَانِ التَّمْرُ وَالمَاءُ، إِلاَّ أنَّهُ قَدْ كَانَ لرسول الله – صلى الله عليه وسلم – جِيرَانٌ مِنَ الأَنْصَارِ، وكَانَتْ لَهُمْ مَنَائِحُ وَكَانُوا يُرْسِلُونَ إِلَى رسول الله – صلى الله عليه وسلم – مِنْ ألْبَانِهَا فَيَسْقِينَا.      متفقٌ عَلَيْهِ


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Urwah ameeleza kuwa ‘Âisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikuwa akimwambia: “Ee mpwa (mtoto wa ndugu wa kiume au wa ndugu kike) wangu, tulikuwa Wallahi tukiutazama mwezi (mwandamo), kisha mwezi mwengine kisha mwezi mwengine, miandamo mitatu katika miezi miwili na ilihali katika nyumba za Mtume ﷺ hakujawashwa moto.” Nikamwuliza: “Ee khalati yangu, mlikuwa mkiishi vipi?” Akajibu: “Kwa vyeusi viwili: tende na maji. Ispokuwa Mtume ﷺ alikuwa ana jirani wa ki-Ansari walikuwa wana mbuzi na walikuwa wakimletea Mtume ﷺ maziwa yake naye akitunywisha.”  [Wameafikiana Bukhari na Muslim.]


Begin typing your search above and press return to search.