باب الخوف
وعن المقداد – رضي الله عنه -، قَالَ: سمِعْتُ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -، يقول: {تُدْنَى الشَّمْسُ يَوْمَ القِيَامَةِ مِنَ الخَلْقِ حَتَّى تَكُونَ مِنْهُمْ كَمِقْدَارِ مِيلٍ} قَالَ سُلَيْم بنُ عامِر الراوي عن المقداد: فَوَاللهِ مَا أدْرِي مَا يعني بالمِيلِ، أمَسَافَةَ الأرضِ أَمِ المِيلَ الَّذِي تُكْتَحَلُ بِهِ العَيْنُ؟ قَالَ: {فَيكُونُ النَّاسُ عَلَى قَدْرِ أعْمَالِهِمْ في العَرَقِ، فَمِنْهُمْ مَنْ يَكُونُ إِلَى كَعْبَيْهِ، ومنهم من يكون إِلَى ركبتيه، ومنهم مَنْ يَكُونُ إِلَى حِقْوَيْهِ، وَمِنْهُمْ مَنْ يُلْجِمُهُ العَرَقُ إلْجَاماً}. قَالَ: وَأَشَارَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – بيدهِ إِلَى فِيهِ. رواه مسلم.
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Al-Miqdâd (Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: “Nilimsikia Mtume ﷺ akisema: [ Siku ya Qiyama jua litaletwa karibu na viumbe hata liwe umbali wa meli moja. Sulaim bin Âmir aliyeipokea Hadîth hii kutoka kwa al-Miqdâd amesema: Wallahi sifahamu anachokusudia katika meli moja, ni masafa ya ardhini ama ni uti wa wanja wa kupakia machoni! Watu watakuwa kulingana na amali zao katika jasho, kuna atakayefikiwa na jasho hadi vifundoni mwake (vya miguu), muna atakayefikiwa hadi magotini mwake, muna atakayefikiwa hadi kiunoni mwake na muna atakayefikiwa hadi mdomoni mwake kabisa, Mtume ﷺ akaashiria mdomoni mwake.”] [ Imepokewa na Muslim. ]