0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

401. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Kumuogopa Mwenyezi Mungu

 باب الخوف


وعن أنس – رضي الله عنه -، قَالَ: خطبنا رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – خطبة مَا سَمِعْتُ مِثلها قطّ، فَقَالَ: {لَوْ تَعْلَمُونَ مَا أعْلَمُ، لَضحِكْتُمْ قَلِيلاً وَلَبَكَيتُمْ كَثِيراً} فَغَطَّى أصْحَابُ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – وَجُوهَهُمْ، وَلَهُمْ خَنَينٌ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

وفي رواية: بَلَغَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – عَنْ أَصْحَابِهِ شَيْءٌ فَخَطَبَ، فَقَالَ: {عُرِضَتْ عَلَيَّ الجَنَّةُ وَالنَّارُ، فَلَمْ أرَ كَاليَومِ في الخَيرِ وَالشَّرِّ، وَلَوْ تَعْلَمونَ مَا أعلَمُ لَضَحِكْتُمْ قَلِيلاً وَلَبَكَيْتُمْ كَثِيراً} فَمَا أتَى عَلَى أصْحَابِ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – يَوْمٌ أَشَدُّ مِنْهُ، غَطَّوْا رُؤُسَهُمْ وَلَهُمْ خَنِينٌ

{الخَنِينُ} بالخاءِ المعجمة: هُوَ البُكَاءُ مَعَ غُنَّة وانتِشَاقِ الصَّوْتِ مِنَ الأنْفِ


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Mtume alituhutubia khutba ambayo sijawahi katu kusikia khutba kama hiyo, akasema: [ Lau mngalikuwa mnayajua ninayoyajua, mngalicheka kidogo na mkalia sana!” Maswahaba wa Mtume ﷺ wakazifunika nyuso zao huku wanalia (kwa king’ong’o).]   [ Wameafikiana Bukhari na Muslim. ]

Riwaya nyingine imesema: [ Mtume ﷺ alipata habari fulani kuhusu Maswahaba wake, akahutubia na akasema: “Nimeonyeshwa Pepo na moto, sijawahi kuona siku kama ya leo katika kheri na shari! Na lau mnajua ninayoyajua, mungelicheka kidogo na mukalia sana!” Basi hakuna siku iliokuwa nzito kwa Maswahaba wa Mtume ﷺ kama siku hiyo, walifunika nyuso zao huku wanalia (kwa king’ong’o).


Begin typing your search above and press return to search.