AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Kufariki kwa Abu Twalib: Abu Twalib aliugua na hakuishi muda mrefu baada ya hapo. Kikamjia kifo chake. Alifariki mnamo mwezi wa Rajab mwaka wa kumi wa Utume. Ilikuwa ni miezi sita baada ya kutoka katika bonde walilotengwa. Aidha inasemekana: alikufa katika mwezi wa Ramadhani kabla ya kufa kwa Bi Khadija (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwa siku tatu?“ (1)
Katika hadithi sahihi kutoka kwa Al-Musaiyab: Inasemwa kuwa Abu Twalib akiwa kitandani mahututi, Mtume (ﷺ) na hali ya kuwa mbele yake yuko Abu Jahli akasema: [Ewe ammi yangu, sema: Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwényezi Mungu (ﷻ), tamko ambalo nitakusogeza kwako mbele ya Mwenyezi Mungu (ﷻ), ] Abu Jahli na Abdillah bin Abu Umayya, walikuwa pale wakasema kumwambia: “Ewe Abu Twalib unaichukia mila ya Abdul Muttwalib? Hawakuacha kuwa wanamsemesha mpaka likawa jambo la mwisho ambalo alilowaambia ni kuwathibitishia kuwa anafuata mila ya ‘Abdul Muttwalib. Mtume (ﷺ) akasema, ”Nitakuombea msamaha mpaka Allah Atakapanikataza kufanya hivyo.”
Ndipo Allah (ﷻ) Afiposhusha aya hii:
مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَن يَسۡتَغۡفِرُواْ لِلۡمُشۡرِكِينَ وَلَوۡ كَانُوٓاْ أُوْلِي قُرۡبَىٰ مِنۢ بَعۡدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمۡ أَنَّهُمۡ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَحِيمِ
[ Haimpasii Nabii na wale walio amini kuwatakia msamaha washirikina, ijapo kuwa ni jamaa zao, baada ya kwisha bainika kuwa hao ni watu wa Motoni.] (9:113)
Na ikashuka:
إِنَّكَ لَا تَهۡدِي مَنۡ أَحۡبَبۡتَ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يَهۡدِي مَن يَشَآءُۚ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ
[Kwa hakika wewe humwongoi umpendaye, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na Yeye ndiye anawajua zaidi waongokao.] (28:56) (2)
Hakuna haja ya kuzungumzia zaidi lile ambalo alikuwa akilifanya Abu Twalib katika kumhami Mtume (ﷺ) kwani alikuwa kama ngome ambayo Uislam na Waislam walijikinga na mashambulizi ya Makuraishi na wajinga, isipokuwa yeye aliendelea kufuata mila za wazee na babu zake, hakusilimu. Hakufaulu moja kwa moja kwani imepokewa katika hadithi sahih kutoka kwa Ibn Abbas bin Abdul Muttwalib aliwahi kusema kumwambia Mtume (ﷺ): ”Hukuweza kumsaidia ammi yako, ijapokuwa alikuwa akikuhami, akikutetea na akighadhibika kwa ajili yako”, Mtume (ﷺ) akasema, [ Yeye yumo motoni, na kama si mimi angekuwa katika walio chini kabisa motoni. ] (3)
Imepokewa kutoka kwa Abu Saeed Al-Khudryi kuwa alimsikia Mtumé (ﷺ)’ akimtaja ammi yake, akasema: [Huenda akanufaika na uombezi wangu siku ya Kiyama, na kwa hivyo akawekwa mahali palipo karibu na kina cha moto, utakaofikia katikafimdo za miguu yake ( nguyu). “(4)