باب فضل بر أصدقاء الأب والأم والأقارب والزوجة وسائر من يندب إكرامه
وعن عبد الله بن دينار، عن عبد الله بن عمر – رضي الله عنهما -: أنَّ رَجُلاً مِنَ الأعْرَابِ لَقِيَهُ بطَريق مَكَّةَ، فَسَلَّمَ عَلَيهِ عبدُ الله بْنُ عُمَرَ، وَحَمَلَهُ عَلَى حِمَارٍ كَانَ يَرْكَبُهُ، وَأعْطَاهُ عِمَامَةً كَانَتْ عَلَى رَأسِهِ، قَالَ ابنُ دِينَار: فَقُلْنَا لَهُ: أصْلَحَكَ الله، إنَّهُمُ الأعرَابُ وَهُمْ يَرْضَوْنَ باليَسير، فَقَالَ عبد الله بن عمر: إن أَبَا هَذَا كَانَ وُدّاً لِعُمَرَ بنِ الخطاب – رضي الله عنه -، وإنِّي سَمِعتُ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -، يقول: {إنَّ أبرَّ البِرِّ صِلَةُ الرَّجُلِ أهْلَ وُدِّ أبِيهِ}
وفي رواية عن ابن دينار، عن ابن عمر: أنَّهُ كَانَ إِذَا خَرَجَ إِلَى مَكّةَ كَانَ لَهُ حِمَارٌ يَتَرَوَّحُ عَلَيهِ إِذَا مَلَّ رُكُوبَ الرَّاحِلةِ، وَعِمَامَةٌ يَشُدُّ بِهَا رَأسَهُ، فَبيْنَا هُوَ يَوماً عَلَى ذلِكَ الحِمَارِ إِذْ مَرَّ بِهِ أعْرابيٌّ، فَقَالَ: ألَسْتَ فُلاَنَ بْنَ فُلاَن؟ قَالَ: بَلَى. فَأعْطَاهُ الحِمَارَ، فَقَالَ: ارْكَبْ هَذَا، وَأعْطَاهُ العِمَامَةَ وَقالَ: اشْدُدْ بِهَا رَأسَكَ، فَقَالَ لَهُ بعضُ أصْحَابِهِ: غَفَرَ الله لَكَ أعْطَيْتَ هَذَا الأعْرَابيَّ حِمَاراً كُنْتَ تَرَوَّحُ عَلَيهِ، وعِمَامةً كُنْتَ تَشُدُّ بِهَا رَأسَكَ؟ فَقَالَ: إنِّي سَمِعتُ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -، يَقُولُ: {إنَّ مِنْ أبَرِّ البِرِّ أنْ يَصِلَ الرَّجُلُ أهْلَ وُدِّ أبيهِ بَعْدَ أنْ يُولِّيَ} وَإنَّ أبَاهُ كَانَ صَديقاً لعُمَرَ – رضي الله عنه
رَوَى هذِهِ الرواياتِ كُلَّهَا مسلم
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa ‘Abdullâh bin Dînâr amepokea kutoka kwa ‘Abdullâh bin ‘Umar Radhi za Allah ziwe juu yao amesimulia: “Mtu mmoja katika mabedui alikutana naye katika njia ya Makkah. ‘Abdullâh bin ‘Umar Radhi za Allah ziwe juu yao akamsalimia, akambeba juu ya punda aliyekuwa akimpanda na akampa kilemba alichokuwa amekivaa kichwani mwake. Ibni Dînâr anaeleza: “Tukamwambia: “Allâh Akusuluhishe, wale ni mabedui, wao huridhika kwa kupewa kitu kidogo tu.” ‘Abdullâh bin ‘Umar akawaambia: “Baba yake alikuwa ni kipenzi cha ‘Umar bin al-Khattâb Radhi za Allah ziwe juu yao. Nami nilimsikia Mtume ﷺ akisema: [ Hakika wema mkubwa ni mtu kuwaunga vipenzi wa baba yake.]
Riwaya nyingine iliopokewa kutoka kwa Ibni Dînâr, inasema: Abdullâh bin Umar alikuwa anapoelekea Makkah alikuwa ana punda akimpanda wakati akichoka kupanda ngamia, na alikuwa ana kilemba alichokuwa akijifunga kichwani mwake. Siku moja alipokuwa yuko juu ya punda, kwa ghafula akapita mbedui, akamwuliza: Wewe si ni fulani bin fulani? Akamjibu: Ndio. Akampa punda, na akamwambia: Mpande huyu, na akampa kilemba na akamwambia: Jifunge kichwa chako kwa hiki. Rafiki yake akamwuliza: Allâh Akusamehe! Umempa mbedui huyu punda uliekuwa ukipumzika juu yake na kilemba ulichokuwa ukijifunga nacho kichwani?” Akamwambia: “Nimemsikia Mtume ﷺ akisema: [Hakika wema mkubwa ni mtu kuwaunga wapenzi wa baba yake baada ya kuwa ameshafariki.] Hakika baba yake alikuwa ni rafiki ya ‘Umar Radhi za Allah ziwe juu yae ” [Riwaya zote hizi zimepokewa na Muslim.]