باب تكبير المسافر إِذَا صعد الثنايا وشبهها وتسبيحه إذا هبط الأودية ونحوهاوالنهي عن المبالغة برفع الصوتِ بالتكبير ونحوه
وعن أَبي موسى الأَشعَريِّ رضي اللَّه عنه قَالَ: كنَّا مَع النبيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم في سَفَرٍ، فكنَّا إِذَا أَشرَفْنَا عَلَى وادٍ هَلَّلنَا وكَبَّرْنَا وَارْتَفَعتْ أَصوَاتنا فقالَ النبيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: “يَا أَيُّهَا النَّاسُ ارْبَعُوا عَلى أَنْفُسِكم فَإنَّكم لاَ تَدعونَ أَصَمَّ وَلا غَائِباً. إنَّهُ مَعكُمْ، إنَّهُ سَمِيعٌ قَريبٌ” متفقٌ عَلَيْهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
171. MLANGO WA MSAFIRI KUPIGA TAKBÎR ANAPOPANDA MILIMA NA MFANO WAKE NA KUSABIHI ANAPOTEREMKA KATIKA MABONDE NA MFANO WAKE, NA MAKATAZO YA KUNYANYUA SAUTI KWA TAKBÎR NA MFANO WAKE
Imepokewa na Abû Mûsâ al-Ash‘ary ( Radhi za Allah ziwe juu yake ) amesimulia: “Tulikuwa pamoja na Mtume ﷺ katika safari fulani. Tukawa tunapopanda (mahala pa juu) hupiga Tahlili, tukapiga Takbir na sauti zetu zikiwa juu. Mtume ﷺ akasema: “Enyi watu! Jihurumieni, hakika nyinyi hamumuombi kiziwi wala aliye mbali, Yeye Yu pamoja nanyi, Yeye ni Mwenye kusikia Aliye karibu.” [ Wameafikiana Bukhari Muslim ]
.