0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

977. Riyadhu Swalihina Mlango wa msafiri kupiga Takbiri unapopanda mlima na mfano wake na kuleta Tasbihi anapo teremka katika Bonde na mfano wake….

باب تكبير المسافر إِذَا صعد الثنايا وشبهها وتسبيحه إذا هبط الأودية ونحوهاوالنهي عن المبالغة برفع الصوتِ بالتكبير ونحوه


وعن ابن عُمر رضي اللَّه عنهما قَالَ: كانَ النَّبِيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم إِذَا قَفَل مِنَ الحجِّ أَو العُمْرَةِ كُلَّما أَوْفى عَلى ثَنِيَّةٍ أَوْ فَدْفَد كَبَّر ثَلاثاً، ثُمَّ قَالَ: “لاَ إلهَ إلاَّ اللَّه وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْك ولَهُ الحمْدُ، وَهُو عَلَى كلِّ شَيءٍ قَدِيرٌ. آيِبُونَ تَائِبُونَ عابِدُونَ ساجِدُونَ لِرَبِّنَا حَامِدُونَ. صدقَ اللَّه وَعْدهُ، وَنَصر عبْده، وَهَزَمَ الأَحزَابَ وحْدَه”        متفقٌ عَلَيْهِ.


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



171. MLANGO WA MSAFIRI KUPIGA TAKBÎR ANAPOPANDA MILIMA NA MFANO WAKE NA KUSABIHI ANAPOTEREMKA KATIKA MABONDE NA MFANO WAKE, NA MAKATAZO YA KUNYANYUA SAUTI KWA TAKBÎR NA MFANO WAKE


Imepokewa na ‘Abdullâh bin ‘Umar ( Radhi za Allah ziwe juu yao ) amesimulia: “Mtume   alikuwa anaporudi kutoka Hajj au ‘Umra kila anapopanda mlima au sehemu ilionyanyuka hupiga Takbîr mara tatu, kisha husema: “Lâ ilâha illallâhu wahdahû lâ sharîka lah, lahulmulku walahulhamdu wahuwa ‘alâ kulli shai-in qadîr. Âyibûna tâ-ibûna ‘âbidûna sâjidûna lirabbinâ hâmidûn, sadaqallâhu wa’dah, wanasara ‘abdah, wahazamal-ahzâba wahdah. [Hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allâh Peke Yake, Ufalme ni Wake na himdi ni Zake, Naye ni Muweza juu ya kila jambo. Tumerejea hali ni wenye kutubia wenye kumuabudu na kumsujudia Mola wetu na kumhimidi. Allâh Amesadikisha waadi Wake, Akamnusuru mja Wake na Akayashinda majeshi Peke Yake._”    [ Wameafikiana Bukhari na Muslim ].


Begin typing your search above and press return to search.