0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

974. Riyadhu Swalihina Mlango wa Anayosema mtu wakati anapopanda mnyama wake wa safari

 باب ما يقوله إذا ركب الدابة للسفرِ


وعن علِيِّ بن ربيعة قَالَ: شَهدْتُ عليَّ بن أَبي طالب رَضي اللَّه عنهُ أُتِيَ بِدابَّةٍ لِيَرْكَبَهَا، فَلما وضَع رِجْلَهُ في الرِّكابِ قَالَ: بِسْم اللَّهِ، فلَمَّا اسْتَوَى عَلَى ظَهْرها قال: الحْمدُ للَّهِ ثُمَّ قَالَ: {سُبْحَانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَذَا، وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرنينَ، وإنَّا إِلَى ربِّنَا لمُنْقلِبُونَ} [الزخرف: ١٤,١٣] ، ثُمَّ قَالَ: الحمْدُ للَّهِ ثَلاثَ مرَّاتٍ، ثُمَّ قَالَ: اللَّه أَكْبرُ ثَلاثَ مرَّاتٍ، ثُمَّ قَالَ: سُبْحانَكَ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي فَاغْفِرْ لِي فإِنَّه لاَ يغْفِرُ الذُّنُوب إِلاَّ أَنْتَ، ثُمَّ ضحِك، فَقِيل: يَا أمِير المُؤْمِنينَ، مِنْ أَيِّ شَيءٍ ضَحِكْتَ؟ قَالَ: رأَيتُ النبيَّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فَعل كَما فعلْتُ، ثُمَّ ضَحِكَ فقلتُ: يَا رسول اللَّهِ مِنْ أَيِّ شَيء ضحكْتَ؟ قال: ” إِنَّ رَبَّك سُبْحانَهُ يَعْجب مِنْ عَبْده إِذَا قَالَ: اغْفِرِ لِي ذنُوبي، يَعْلَمُ أَنَّهُ لاَ يغْفِرُ الذَّنُوبَ غَيْرِي”رواه أَبو داود، والترمذي وَقالَ: حديثٌ حسنٌ، وفي بعض النسخ: حسنٌ صحيحٌ. وهذا لفظ أَبي داود


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



170. MLANGO WA ANAYOSEMA MTU WAKATI ANAPOMPANDA MNYAMA WAKE WA SAFARI


Imepokewa na ‘Alî bin Rabî‘ah amesimulia: “Nilimuona ‘Alî bin Abîtâlib  ( Radhi za Allah ziwe juu yake ) akiletewa mnyama ili ampande, alipouweka mguu wake katika kikuku (cha kupandia farasi) alisema: “Bismillâh [Kwa Jina la Allâh]. Alipoketi sawa juu ya mgongo wake alisema: “Subhânalladhî sakkhara lanâ hâdhâ wamâ kunnâ lahû muqrinîn, wa innâ ilâ rabbinâ lamunqalibûn [Ametakasika Aliyemfanya huyu atutumikie, na tusingeliweza kufanya haya wenyewe na hakika sisi tutarudi kwa Mola wetu Mlezi._” Kisha akasema: “Alhamdulillâh, [Kila jinsi ya sifa njema ni ya Allâh].” mara tatu, kisha akasema: “Allâhu Akbar, [Allâh ni Mkubwa].” mara tatu, kisha akasema: “Subhânaka innî dhwalamtu nafsî faghfirlî fa-innahû lâ yaghfiruddhunûba illâ anta, [Kutakasika ni Kwako, hakika mimi nimeidhulumu nafsi yangu, Nisamehe, hakika hakuna mwenye kusamehe dhambi ila ni Wewe].” Kisha akacheka. Akaulizwa: “Ewe Amiri wa Waumini, wacheka jambo gani?” Akajibu: “Nilimuona Mtume ﷺ akifanya kama nilivyofanya, kisha akacheka, nikamwuliza: “Yâ Rasûlallâh, umecheka jambo gani?” Akanijibu: “Hakika Mola wako – Aliyetakasika – Hupendezwa na mja Wake wakati anaposema: “Nisamehe dhambi zangu, yeye anajua kuwa hakuna anayesamehe dhambi ila Mimi (Allâh).”   [ Imepokewa na Abû Dâwûd na Tirmidhy, na amesema: Hadîth hii ni Hasan.]


Begin typing your search above and press return to search.