بابُ إعانةِ الرفيقِ
وعنْ جابرٍ رضيَ اللَّه عنهُ، عَنْ رسولِ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم أَنَّه أَرادَ أَنْ يَغْزُوَ فَقَالَ: “يَا معْشَرَ المُهَاجِرِينَ والأنصارِ، إِنَّ مِنْ إخوَنِكُم قَوْماً، ليْس لهمْ مَالٌ، وَلا عشِيرَةٌ، فَلْيَضُمَّ أَحَدكم إِليْهِ الرَجُلَيْنِ أَوِ الثَّلاثَةَ،” فَمَا لأحدِنَا منْ ظهرٍ يحْمِلُهُ إلا عُقبَةٌ يعْني كَعُقْبَةٍ أَحَدهمْ، قال: فَضَممْتُ إليَّ اثْنَيْينِ أَو ثَلاثَةً مَا لِي إِلاَّ عُقبةٌ كعقبَةِ أَحَدِهمْ مِنْ جَملي. رواه أَبُو داود
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
169. MLANGO WA KUMSAIDIA SAHIBA KATIKA SAFARI
Imepokewa kutoka kwa Jâbir ( Radhi za Allah ziwe juu yake ) amesimulia kuwa Mtume ﷺ alitaka kwenda kupigana (Jihadi), akasema: “Enyi mkusanyiko wa Muhajirina na Ansari! Hakika katika ndugu zenu muna watu wasio na mali wala kabila (la kuwasaidia), basi mmoja wenu awape matumizi watu wawili au watatu.” Kila mmoja wetu akawa anapanda kwa zamu sawa na mwenzie. Mimi niliwachukua watu wawili au watatu, basi nikipanda sawa na wao katika ngamia wangu.” [ Imepokewa na Abû Dâwûd.]