بابُ إعانةِ الرفيقِ
وعن أَبي سعيدٍ الخُدْريِّ رَضيَ اللَّه عنه قَالَ: بَيْنَمَا نَحْنُ في سَفَرٍ إِذ جَاءَ رَجُلٌ عَلَى رَاحِلةٍ لهُ، فَجعَلَ يَصْرِفُ بَصَرهُ يَمِيناً وَشِمَالاً، فَقَالَ رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: “مَنْ كَانَ مَعَهُ فَضْلُ ظَهرٍ، فَلْيعُدْ بِهِ عَلَى منْ لا ظَهر لَهُ، ومَنْ كانَ لَهُ فَضلُ زَادٍ، فَلْيَعُدْ بِهِ عَلى مَنْ لا زَادَ لَهُ” فَذَكَرَ مِنْ أَصْنافِ المَالِ مَا ذَكَرَهُ، حَتى رَأَينَا أَنَّهُ لاَ حقَّ لأحَدٍ مِنَّا في فضْلٍ. رواه مسلم
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
169. MLANGO WA KUMSAIDIA SAHIBA KATIKA SAFARI
Imepokewa kutoka kwa Abû Sa‘îd al-Khudry ( Radhi za Allah ziwe juu yake ) amesimulia: “Tulipokuwa safarini pamoja na Mtume ﷺ , mara akaja mtu aliyepanda mnyama wake, akawa anatazama kulia na kushoto. Mtume ﷺ akasema: “Mwenye mnyama wa ziada ampe sadaka asiye na mnyama, na mwenye akiba ya ziada, ampe asie na akiba.” Akataja aina kadhaa za mali kiasi aliyotaja mpaka tukadhani kuwa hakuna haki kwa yeyote miongoni mwetu kubaki na ziada ya kitu.” [ Imepokewa na Muslim. ]