باب آداب السير والنزول والمبيت والنوم في السفر واستحباب السُّرَى والرفق بالدواب ومراعاة مصلحتها وجواز الإرداف عَلَى الدابة إِذَا كانت تطيق ذلك وأمر من قصّر في حقها بالقيام بحقها
وعَن أَبي جعفرٍ عبدِ اللَّهِ بنِ جعفرٍ، رضيَ اللَّه عنهما قَالَ: أَرْدفني رَسُول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم، ذَاتَ يَوْم خَلْفَه، وَأسَرَّ إِليَّ حدِيثاً لا أُحَدِّث بِهِ أحَداً مِنَ النَّاسِ، وكانَ أَحبَّ مَا اسْتَتَر بِهِ رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم لِحاجَتِهِ هَدَفٌ أَوْ حَائشُ نَخل. يَعْني: حَائِطَ نَخْل: رواه مسلم هكذا مختصراً
وزادَ فِيهِ البَرْقانيُّ بإِسناد مسلم: بعد قَوْله: حائشُ نَخْلٍ: فَدَخَلَ حَائطاً لِرَجُلٍ منَ الأَنْصارِ، فَإذا فِيهِ جَمَلٌ، فَلَمَّا رَأى رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم جرْجرَ وذَرفَتْ عَيْنَاه، فأَتَاهُ النبيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فَمَسَحَ سَرَاتَهُ أَي: سنامَهُ وَذِفْرَاهُ فَسكَنَ، فَقَالَ: “مَنْ رَبُّ هَذَا الجَمَلِ، لِمَنْ هَذا الجَمَلُ؟ “فَجاءَ فَتى مِنَ الأَنصَارِ فقالَ: هَذَا لِي يَا رسولَ اللَّه. فقالَ:”أَفَلا تَتَّقِي اللَّه في هذِهِ البَهيمَةِ الَّتي مَلَّكَكَ اللَّهُ إياهَا؟ فإنَّهُ يَشْكُو إِليَّ أَنَّكَ تُجِيعُهُ وَتُدْئِبُهُ “. ورواه أَبُو داود كروايةِ البَرْقاني
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
168. MLANGO WA NIDHAMU ZA MWENDO (SAFARINI), KUTEREMKIA, KULALA SAFARINI, NA SUNNAH YA KUSAFIRI USIKU, KUWATENDEA UPOLE WANYAMA, KUCHUNGA MASLAHI YAO, KUMUAMURU ANAYEKUSURU KATIKA HAKI YAO KUWAPA HAKI ZAO NA KUFAA KUMPANDISHA MTU NYUMA YA MNYAMA IWAPO MNYAMA YULE ATAWEZA KUWABEBA WOTE
Imepokewa kutoka Abû Ja’far, ‘Abdullâh bin Ja’far ( Radhi za Allah ziwe juu yake ) amesimulia: “Siku moja Mtume ﷺ alinipandisha nyuma ya mnyama wake, akanizungumzia mazungumzo ya siri ambayo sitamweleza yeyote. Na ilikuwa kinachompendeza mno kujisitiri nacho Mtume ﷺ anapokidhi haja, ilikuwa ni kitu kilichonyanyuka au bustani ya mtende.” [ Imepokewa na Muslim ] .
al-Barqâny ameongezea kwa isnadi ya Muslim: “..akaingia katika bustani la bwana mmoja wa ki-Ansari, ndani yake ikawa muna ngamia, yule ngamia alipomuona Mtume ﷺ alitoa sauti na macho yake yakabubujikwa machozi. Mtume ﷺ akamwendea, akampangusa nundu yake na nyuma ya masikio yake, akatulia. (Mtume ﷺ) akauliza: “Ni nani mwenye ngamia huyu? Ngamia huyu ni wa nani?” Akaja kijana wa ki-Ansari akasema: “Huyu ni wangu Yâ Rasûlallâh.” Akamwambia: “Humchi Allâh katika mnyama huyu ambaye Allâh Amekumilikisha? Yeye amenishitakia kuwa unamwacha na njaa na unamtaabisha.” Vile vile [ Imepokewa na Abû Dâwûd ameipokea kama ile riwaya ya al-Barqâny.]