0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

151. MLANGO WA ANAYOSEMA MTU BAADA YA KUMFUMBA MACHO MAITI

 باب مَا يقوله بعد تغميض الميت


عن أُمِّ سَلمةَ رضيَ اللَّهُ عنها قالت: دَخَلَ رسُولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم عليّ أَبي سلَمة وَقَدْ شَقَّ بصَرُهُ، فأَغْمضَهُ، ثُمَّ قَال: “إِنَّ الرُّوح إِذا قُبِضَ، تبِعَه الْبصَرُ” فَضَجَّ نَاسٌ مِنْ أَهْلِهِ فَقَالَ: “لاَ تَدْعُوا عَلى أَنْفُسِكُم إِلاَّ بِخَيْرٍ، فإِنَّ المَلائِكَةَ يُؤمِّنُون عَلى مَا تَقُولونَ” ثمَّ قالَ:”اللَّهُمَّ اغْفِر لأَبِي سَلَمَة، وَارْفَعْ درَجَتهُ في المَهْدِيِّينَ، وَاخْلُفْهُ في عَقِبِهِ في الْغَابِرِين، واغْفِرْ لَنَا ولَه يَاربَّ الْعَالمِينَ، وَافْسحْ لَهُ في قَبْرِهِ، وَنَوِّرْ لَهُ فِيهِ ”       رواه مسلم


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



151. MLANGO WA ANAYOSEMA MTU BAADA YA KUMFUMBA MACHO MAITI


Imepokewa na Ummu Salamah  (Radhi za Allah ziwe juu yake)  amesimulia: “Mtume ﷺ aliingia nyumbani mwa Abû Salamah na alikuwa amekodoa macho yake, akamfumba na akasema: “Kwa yakini roho inapochukuliwa huandamwa na macho.” Watu katika jamaa zake wakaangua kilio kikubwa. Akawaambia: “Msijiombee ela kheri, hakika Malaika wanaitikia Amin kwa mnayosema.” Kisha akaomba: “Allâhummagh-fir li abî salamah, warfa’ darajatahû fil-mahdiyyîn, wakhlufhu fî ‘aqibihî fil-ghâbirîn, waghfir lanâ walahû yâ rabbal-‘âlamîn, wafsah lahû fî qabrih, wanawwir lahû fîh. [Ewe Mola Msamehe Abû Salamah, Umnyanyue daraja yake katika waongofu, Uwe badala yake kwa vizazi vyake, Utusamehe sisi na yeye Ewe Mola wa viumbe, Umkunjulie kaburini mwake na Umng’arishie].”    [ Imepokea na Muslim.]


Begin typing your search above and press return to search.