0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

951. Riyadhu Swalihina Mlango wa Watu kumsifu maiti

باب ثناء الناس عَلَى الميت


 وعن أَبي الأسْوَدِ قَالَ: قَدِمْتُ المدِينَةَ، فَجَلَسْتُ إِلَى عُمْرَ بنِ الخَطَّابِ رضي اللَّه عنْهُ فَمرَّتْ بِهِمْ جنَازةٌ، فأُثنىَ عَلَى صَاحِبها خَيْراً فَقَالَ عُمَرُ: وَجَبَتْ، ثُمَّ مُرَّ بأُخْرى، فَأثنِىَ عَلَى صَاحِبِها خَيراً، فَقَالَ عُمرُ: وجبَت، ثُمَّ مُرَّ بِالثَّالِثَةِ، فَأُثنِيَ عَلَى صَاحِبِهَا شَرًّا، فَقَال عُمرُ: وجبتْ: قَالَ أَبُو الأسْودِ: فَقُلْتُ: وَمَا وجبَت يَا أميرَ المُؤمِنينَ؟ قَالَ: قُلتُ كما قَالَ النَّبيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: “أَيُّمَا مُسلِم شَهِدَ لهُ أَربعةٌ بِخَير، أَدخَلَهُ اللَّه الجنَّةَ”فَقُلنَا: وثَلاثَةٌ؟ قَالَ:”وثَلاثَةٌ”فقلنا: واثنانِ؟ قال:”واثنانِ” ثُمَّ لم نَسأَ لْهُ عَن الواحِدِ.      رواه البخاري


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



163. MLANGO WA WATU KUMSIFU MAITI


Imepokewa na Abul-aswad ad-Daily amesimulia: “Nilikuja Madina, nikaketi na ‘Umar bin al-Khattâb  (Radhi za Allah ziwe juu yake), jeneza likapita, yule maiti akasifiwa kwa wema. ‘Umar akasema: “Limepasa.” Kisha likapita jeneza la pili, yule maiti akasifiwa kwa wema. ‘Umar akasema: “Limepasa.” Kisha likapita jeneza la tatu, yule maiti akasifiwa kwa ubaya. ‘Umar akasema: “Limepasa.” Nikamwuliza: “Ni kitu gani kilichopasa ewe Amiri wa Waumini?” Akajibu: “Nimesema kama alivyosema Mtume ﷺ : “Muislamu yeyote atakayeshuhudiwa wema na watu wanne, Allâh Atamuingiza Peponi.” Tukamwuliza: “Na watu watatu (wakimshuhudia kwa wema)?” Akajibu: “Na watu watatu pia.” Tukamwuliza: “Na watu wawili?” Akajibu: “Na watu wawili pia.” Wala hatukumwuliza kuhusu mtu mmoja.”  [ Imepokewa na Bukhari ].


Begin typing your search above and press return to search.