0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

95. MLANGO WA SUNNAH YA KUTOA BISHARA NJEMA NA KUPONGEZA KHERI

باب استحباب التبشير والتهنئة بالخير


قَالَ الله تَعَالَى: ﴿فَبَشَّرْ عبادِ الذينَ يَسْتَمِعُونَ القَوْلَ فيتَّبِعُونَ أَحْسَنهُ﴾ [ الزمر: 17-18 ]

وقال تَعَالَى: ﴿يُبَشِّرُهُمْ رَبُّهُمْ بِرَحْمَةٍ مِنْهُ وَرِضْوانٍ وَجَنَّاتٍ لَهُمْ فِيهَا نَعِيمٌ مُقِيمٌ﴾ [ التوبة: 21 ]

وقال تَعَالَى: ﴿وَأَبْشِرُوا بِالجَنَّةِ الَّتي كُنْتُم تُوعَدُونَ﴾ [ فصلت: 30 ]

وقال تَعَالَى: ﴿فَبَشَّرْنَاهُ بِغُلاَمٍ حَلِيمٍ﴾ [ الصافات: 101 ]

وقال تَعَالَى: ﴿وَلَقدْ جَاءتْ رُسُلُنَا إبْراهِيمَ بِالبُشْرَى﴾ [ هود: 69 ]

وقال تَعَالَى: ﴿وَامْرَأَتُهُ قَائِمَةٌ فَضَحِكَتْ فَبَشَّرْنَاهَا بِإِسْحَاقَ وَمِنْ وَرَاءِ إسْحَاقَ يَعْقُوبَ﴾ [ هود: 71 ]

وقال تَعَالَى: ﴿فَنَادَتْهُ المَلاَئِكَةُ وَهُوَ قَائِمٌ يُصَلِّي في المِحْرَابِ أَنَّ اللهَ يُبَشِّرُكَ بِيَحْيَى﴾ [ آل عمران: 39 ]

وقال تَعَالَى: ﴿إِذْ قَالَتِ الْمَلاَئِكَةُ يَا مَرْيَمُ إنَّ اللهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٍ مِنْهُ اسْمُهُ الْمسِيحُ﴾ [ آل عمران: 45 ] الآية

والآيات في الباب كثيرة معلومة


شرح مقدمة عن الباب مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



95. MLANGO WA SUNNAH YA KUTOA BISHARA NJEMA NA KUPONGEZA KHERI


Mwenyezi Mungu Amesema: “Basi wabashirie waja Wangu. Ambao husikiliza maneno, wakafuata lilio bora yao.” [39:17, 18].

Mwenyezi Mungu Amesema: “Mola wao Mlezi Anawabashiria rehema zitokazo Kwake, na Radhi, na Bustani ambazo humo watapata neema za kudumu.” [9:21].

Mwenyezi Mungu Amesema: “Nanyi furahini kwa Pepo mliyokuwa mkiahidiwa.” [41:30].

AMwenyezi Mungu Amesema: “Basi Tukambashiria mwana aliye mpole.” [37:101].

Mwenyezi Mungu Amesema: “Na wajumbe Wetu walimjia Ibrâhîm kwa bishara njema.” [11:69].

Mwenyezi Mungu Amesema: “Na mkewe alikuwa kasimama wima, akacheka. Basi tukambashiria (kuzaliwa) Is-haq, na baada ya Is-haq Yaaqub.” [11:71].

Mwenyezi Mungu Amesema: “Alipokuwa amesimama chumbani akiswali, Malaika akamnadia: Hakika Allâh Anakubashiria Yahya.” [3:39].

Mwenyezi Mungu Amesema: “Na pale Malaika waliposema: Ewe Maryamu! Hakika Allâh Anakubashiria (mwana) kwa Neno litokalo Kwake. Jina lake ni Masihi..” mpaka mwisho wa Aya. [3:45].


Begin typing your search above and press return to search.