0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

944. Riyadhu Swalihina Mlango wa kuharakisha kumlipia Maiti deni lake na kuharakisha kumuandaa kwa Mazishi…

باب تعجيل قضاء الدَّين عن الميت والمبادرة إلى تجهيزه إلا أن يموت فجاءة فيترك حَتَّى يُتَيَقَّنَ مَوْتُه


وعن حُصَيْنِ بن وحْوَحٍ رضي اللَّهُ عنه أَنْ طَلْحَةَ بنَ الْبُرَاءِ بن عَازِبٍ رضِي اللَّه عنْهما مَرِض، فَأتَاهُ النَّبيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يَعُودُهُ فَقَالَ: إنِّي لاَ أُرَى طَلْحةَ إلاَّ قدْ حَدَثَ فِيهِ المَوْتُ فَآذِنُوني بِهِ وَعَجِّلُوا بِهِ، فَإنَّهُ لاَ يَنْبَغِي لجِيفَةِ مُسْلِمٍ أنْ تُحْبَسَ بَيْنَ ظَهْرَانَيْ أَهْلِهِ”.     رواه أَبُو داود


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



159. MLANGO WA KUHARAKISHA KUMLIPIA MAITI DENI LAKE NA KUHARAKISHA KUMWANDAA KWA MAZISHI, ISPOKUWA ATAPOKUFA GHAFLA, HAPO ATAACHWA MPAKA KUTHIBITISHWE KUFA KWAKE


Imepokewa na Husain bin Wahwah (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia kuwa Talha bin al-Barâ bin ‘Âzib (Radhi za Allah ziwe juu yake) aliugua, Mtume akamwendea kumzuru. Kisha akasema: “Mimi nadhani Talha amekaribia kufa, (atakapokufa) nijulisheni na mumharakishe (kumzika), kwa hakika haitakiwi mwili wa Muislamu (aliekufa) kubaki miongoni mwao.”    [ Imepokewa na Abû Dâwûd.]


Begin typing your search above and press return to search.