باب الإِسراع بالجنازة
وعن أَبي سعيدٍ الخُدْرِيِّ رضي اللَّه عنه قَالَ. كَانَ النَّبيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يَقُولُ: “إِذَا وُضِعَتِ الجِنَازَةُ، فَاحْتَملَهَا الرِّجَالُ عَلى أَعنَاقِهِمْ، فَإنْ كَانتْ صَالحةً، قالتْ: قَدِّمُوني، وَإنْ كَانَتْ غَيْرَ صَالِحَةٍ، قَالَتْ لأهْلِهَا: يَاوَيْلَهَا أَيْنَ تَذْهَبُونَ بِهَا، يَسْمَعُ صَوْتَهَا كُلُّ شَيْءٍ إلاَّ الإنسانَ، وَلَوْ سَمِعَ الإنْسَانُ، لَصَعِقَ ” رواه البخاري
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
158. MLANGO WA KUHARAKISHA JENEZA
Imepokewa na Abû Sa‘îd al-Khudry (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Mtume ﷺ alikuwa akisema: “Jeneza linapowekwa na watu wakalibeba juu ya shingo zao, ikiwa yule aliekufa ni mtu mwema, atasema: “Nipelekeni!” Na akiwa si mtu mwema, atawaambia waliolibeba: “Ole wangu! Mwanipeleka wapi?” Kila kitu kitasikia sauti yake ispokuwa mwanadamu, na lau mwanadamu angaliisikia, angalipotewa na fahamu (kutokana na sauti yake jinsi ilivyo kali kwa sababu ya adhabu anayoiyona).” [ Imepokewa na Bukhari ].