باب مَا يقرأ في صلاة الجنازة
وعن واثِلة بنِ الأسقعِ رضيَ اللَّه عنه قَالَ: صَلَّى بِنَا رسولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم عَلى رجُلٍ مِنَ المُسْلِمينَ، فَسَمِعْتُهُ يقولُ: “اللَّهُمَّ إنَّ فُلانَ ابْنَ فُلان في ذِمَّتِكَ وَحَبْلِ جِوَارِكَ، فَقِهِ فِتْنَةَ القَبْر، وَعَذَابَ النَّارِ، وَأَنْتَ أَهْلُ الوَفاءِ والحَمْدِ، اللَّهُمَّ فاغفِرْ لهُ وَارْحَمْهُ، إنكَ أَنْتَ الغَفُور الرَّحيمُ ” رواه أَبُو داود
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
157. MLANGO WA KINACHOSOMWA KATIKA SWALA YA JENEZA
Imepokewa na Wâthilah bin al-‘Asqa’ (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Mtume ﷺ alituswalisha (Swala ya jeneza) ya mmoja katika Waislamu, nikamsikia akiomba: “Allâhumma inna fulân bin fulân fî dhimmatika wa habli jiwârik, faqihî fitnatalqabri wa ‘adhâbannâr, wa anta ahlulwafâ-i walhamd, Allâhumma faghfirlahû warhamhu innaka antalghafûrurrahîm. [Ewe Mola, hakika fulani bin fulani yuko katika Dhima Yako na Himaya ya Ujirani Wako, basi Mkinge na majaribio ya kaburini, na (Umkinge) adhabu ya moto, Nawe Ndiwe Mwenye kutoa na kushukuriwa. Ewe Mola, Msamehe na Umrehemu, hakika Wewe ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu].” [ Imepokewa na Abû Dâwûd.]