باب مَا يقرأ في صلاة الجنازة
وعن أبي هُريْرَةَ رَضِي اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم في الصَّلاةِ عَلى الجَنَازَة: “اللَّهُمَّ أَنْت ربُّهَا، وَأَنْتَ خَلَقْتَها، وأَنْتَ هَديْتَهَا للإسلامِ، وَأَنْتَ قَبَضْتَ رُوحَهَا، وَأَنْتَ أَعْلمُ بِسِرِّها وَعَلانيتِها، جئْنَاكَ شُفعاءَ لَهُ فاغفِرْ لهُ”. رواه أَبُو داود
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
157. MLANGO WA KINACHOSOMWA KATIKA SWALA YA JENEZA
Imepokewa na Abû Huraira amempokea Mtume ﷺ alikuwa akiomba katika Swala ya jeneza: “Allâhumma anta rabbuhâ, wa anta khalaqtahâ, wa anta hadaitahâ lil-islâm, wa anta qabadhta rûhahâ, wa anta a’lamu bi sirrihâ wa ‘alâniyatihâ, ji-nâka shufa‘â-a lah, faghfirlah. [Ewe Mola Wewe Ndiwe Mola wake, Wewe Ndiwe Uliemuumba, Wewe Ndiwe Uliemuongoza katika Uislamu, Wewe Ndiwe Ulieichukua roho yake, Nawe Ndiwe Unaejua siri yake na dhahiri yake, tumekujia ilihali tunamwombea, Msamehe].” [ Imepokewa na Abû Dâwûd.]