[باب مَا يُدعى به للمريض]
وعن أَبي سعيد الخُدْرِيِّ وأَبي هريرة رضيَ اللَّه عنهما، أَنهُما شَهِدَا عَلَى رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم أَنه قالَ:“مَنْ قَالَ: لاَ إِلهَ إِلاَّ اللَّهُ واللَّهُ أَكْبَرُ، صدَّقَهُ رَبَّهُ، فَقَالَ: لاَ إِله إِلاَّ أَنَا وأَنا أَكْبرُ. وَإِذَا قَالَ: لاَ إِلهَ إِلاَّ اللَّهُ وحْدهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، قَالَ: يقول: لاَ إِله إِلا أَنَا وحْدِي لا شَرِيك لِي. وَإِذَا قَالَ: لاَ إِلهَ إِلاَّ اللَّهُ لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ، قَالَ: لاَ إِلهَ إِلاَّ أَنَا ليَ المُلْك وَلىَ الحَمْدُ. وإِذا قَالَ: لاَ إله إِلاَّ اللَّهُ وَلا حَوْلَ وَلاَ قَوَّةِ إِلاَّ بِاللَّهِ، قَالَ لاَ إِله إِلاَّ أَنَا وَلا حَوْلَ وَلاَ قوَّةَ إِلاَّ بي” وَكانَ يقولُ:”مَنْ قالهَا في مَرَضِهِ ثُمَّ ماتَ لَمْ تَطْعَمْهُ النَّارُ” رواه الترمذي وقال: حديث حسن
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
145. MLANGO WA DUA ANAYOOMBEWA MGONJWA
Imepokewwa na Abû Sa‘îd al-Khudry na Abû Huraira (Radhi za Allah ziwe juu yao) wameshuhudia kuwa Mtume ﷺ amesema: “Atakayesema: Lâ ilâha illallâhu wallâhu akbar [Hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allâh, Allâh Ndiye Mkuu_, Mola wake Humsadikisha Akasema: “Hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki ispokuwa Mimi, Nami Ndimi Mkuu.” Atakaposema: “Lâ ilâha illallâhu wahdahû lâ sharîka lah [Hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allâh, ni Yeye Pekee Hana mshirika_, Naye Husema: “Hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki ispokuwa Mimi Peke Yangu Sina mshirika.” Na atakaposema: “Lâ ilâha illallâhu, lahulmulku walahulhamd [Hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allâh, Ufalme ni Wake na Himdi ni Zake_, Allâh Husema: “Hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki ispokuwa Mimi, Ufalme ni Wangu na Himdi ni Zangu.” Atakaposema: “Lâ ilâha illallâhu walâ hawla walâ quwwata illâ billâh [Hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allâh, wala hakuna jinsi ya hila ya kuepuka maasia wala hakuna nguvu ya kufanyia ibada ela kwa msaada wa Allâh_, Allâh Husema: “Hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki ispokuwa Mimi, wala hakuna jinsi ya hila ya kuepuka maasia wala hakuna nguvu ya kufanyia ibada ela kwa msaada Wangu.” Na alikuwa akisema: “Atakayesema maneno hayo katika maradhi yake kisha akafariki, moto hautamchoma.” [ Imepokelewa na Tirmidhy, na amesema: Hadîth hii ni Hasan.]