[باب عيادة المريض]
وعن أَنسٍ، رضي اللَّهُ عنه، قَالَ: كانَ غُلامٌ يَهُودِيٌّ يَخْدُم النَّبيَّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم، فمرِضَ فأَتَاهُ النَّبِيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يعُودهُ، فَقَعَدَ عِنْدَ رَأْسِهِ فقالَ لَهُ: “أَسْلِمْ”فنَظَرَ إِلى أَبِيهِ وهُو عِنْدَهُ؟ فَقَالَ: أَطِعْ أَبا الْقاسِمِ، فَأَسْلَم، فَخَرَجَ النَّبِيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم، وَهُوَ يقولُ:“الحَمْدُ للَّهِ الَّذي أَنْقذهُ مِنَ النَّارِ”. رواه البخاري
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
144. MLANGO WA KUMTEMBELEA MGONJWA, KUSINDIKIZA MAITI (JENEZA), KUMSWALIA, KUHUDHURIA MAZISHI YAKE NA KUKETI KABURINI MWAKE BAADA YA KUMZIKA
Imepokewwa na Anas (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Alikuwepo kijana mmoja wa Kiyahudi aliyekuwa akimhudumikia Mtume ﷺ alishikwa na maradhi. Mtume ﷺ akamzuru, akaketi kichwani mwake, akamwambia: “Silimu.” Akamtizama baba yake naye yuko mbele yake, (baba yake) akamwambia: “Msikilize Abal-Qâsim.” Akasilimu. Mtume ﷺ alipotoka alisema: “Namshukuru Allâh Aliemuokoa na moto!” [ Imepokelewa na Bukhârî.]