[باب عيادة المريض]
وعن عليّ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقُولُ: “مَا مِنْ مُسْلِم يَعُودُ مُسْلِماً غُدْوة إِلاَّ صَلَّى عَلَيْهِ سَبْعُونَ ألْفَ مَلَكٍ حَتَّى يُمْسِي، وَإنْ عَادَهُ عَشِيَّةً إِلاَّ صَلَّى عَلَيْهِ سَبْعُونَ ألْفَ ملكٍ حَتَّى يُصْبحَ، وَكَانَ لَهُ خَرِيفٌ في الْجَنَّةِ” رواه الترمِذِي وقال: حديث حسن
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
144. MLANGO WA KUMTEMBELEA MGONJWA, KUSINDIKIZA MAITI (JENEZA), KUMSWALIA, KUHUDHURIA MAZISHI YAKE NA KUKETI KABURINI MWAKE BAADA YA KUMZIKA
Imepokewwa na ‘Alî (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Nilimsikia Mtume ﷺ akisema: “Muislamu yeyote anayemzuru Muislamu wakati wa asubuhi, huombewa maghfira na Malaika elfu sabiini mpaka anapofika jioni, na akimzuru jioni, huombewa maghfira na Malaika elfu sabiini mpaka apambaukiwe, na atakuwa ana matunda ya Peponi.” [ Imepokelewa na Tirmidhy, na amesema: Hadîth hii ni Hasan.]