[باب عيادة المريض]
وعن أبي هريرة رضي الله وعنه قال قال رسول الله صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: إنَّ اللهَ عزَّ وجل يَقُولُ يَوْمَ القيَامَة: “يَا ابْنَ آدَمَ مَرضْتُ فَلَم تَعُدْني، قال: ياربِّ كَيْفَ أعُودُكَ وأنْتَ رَبُّ العَالَمين؟ قَالَ: أمَا عَلْمتَ أنَّ عَبْدي فُلاَناًَ مَرِضَ فَلَمْ تَعُدْهُ، أمَا عَلمتَ أنَّك لَوْ عُدْته لَوَجَدْتَني عِنْدَهُ؟ يَا ابْنَ آدَمَ اسْتَطْعَمْتُكَ فَلَمْ تُطْعِمنِي، قَالَ: يَا رَبِّ كَيْفَ أطْعِمُكَ وَأنْتَ رَبُّ العَالَمِينَ، قَالَ: أمَا عَلِمْتَ أنَّهُ اسْتَطْعَمَكَ عَبْدِي فُلانٌ فَلَمْ تُطْعِمْهُ أمَا عَلِمْتَ أنَّكَ لَوْ أطْعَمْتَهُ لَوَجَدْتَ ذَلِكَ عِنْدِي؟ يَا ابْنَ آدَمَ اسْتَسْقَيْتُكَ فلم تسقني، قال: يارب كَيْفَ أسْقِيكَ وَأنْتَ رَبُّ العَالَمينَ؟ قَالَ: اسْتَسْقَاكَ عَبْدِي فُلاَنٌ فَلَمْ تَسْقِهِ، أمَا عَلِمْتَ أنَّكَ لو سقيته لو جدت ذَلِكَ عِنْدِي؟ “ رواه مسلم.
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
144. MLANGO WA KUMTEMBELEA MGONJWA, KUSINDIKIZA MAITI (JENEZA), KUMSWALIA, KUHUDHURIA MAZISHI YAKE NA KUKETI KABURINI MWAKE BAADA YA KUMZIKA
Imepokewwa na Abû Huraira (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Mtume ﷺ amesema: “Kwa yakini Allâh ‘Azza wa Jalla Siku ya Qiyama Atasema: “Ewe mwanadamu, Niliugua wala hukunizuru!” (Mwanadamu atauliza kwa mshangao): “Ewe Rabbi, vipi nikuzuru Nawe Ni Mola wa viumbe vyote?” Atamwambia: “Kwani hukujua kuwa mja Wangu fulani aliugua wala hukumzuru, kwani hukujua kuwa lau ungalimzuru ungalinikuta kwake?” “Ewe mwanadamu, Nilikuomba chakula wala hukunilisha!” Atauliza: “Ewe Rabbi, vipi nikulishe ilihali Wewe Ndiwe Mola wa viumbe vyote?” Atamwambia: “Kwani hukujua kuwa mja Wangu fulani alikuomba chakula wala hukumlisha? Kwani hukujua kuwa lau ungalimlisha malipo ya kitendo hicho ungaliyakuta Kwangu?” “Ewe mwanadamu, Nilikuomba maji hukunipa!” Atauliza: “Ewe Rabbi, vipi nitakunywisha maji Nawe Ndiye Mola wa viumbe vyote?” Atamwambia: “Mja Wangu fulani alikuomba maji wala hukumpa, kwani hukujua kuwa lau ungalimpa maji malipo ya kitendo hicho ungaliyakuta Kwangu?” [ Imepokelewa na Muslim ].