باب استحباب المصافحةِ عندَ اللقاء وبشاشةِ الوجهِ وتقبيل يد الرجل الصالح وتقبيل ولده شفقة ومعانقة القادم من سفر وكراهية الانحناء
وعن أنس رضي الله عنه قَالَ: لَمَّا جَاءَ أهْلُ اليَمنِ قَالَ رسولُ الله صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: “قَدْ جَاءَكُمْ أهْلُ الْيَمَنِ، وَهُمْ أولُ مَنْ جَاءَ بالمُصَافَحَة” رواه أَبُو داود بإسناد صحيح
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
143. MLANGO WA SUNNAH YA KUPEANA MIKONO WAKATI WA KUKUTANA, KUWA NA USO WA BASHASHA, KUUBUSU MKONO WA MTU MWEMA, MTU KUMBUSU MWANAWE KWA HURUMA, KUMPIGA MAKAMAMA ALIEKUJA KUTOKA SAFARINI NA UKARAHA WA KUINAMA
Imepokewwa na Anas (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Watu wa Yemen walipokuja, Mtume ﷺ alisema: “Mmejiliwa na watu wa Yemen”, nao ndio watu wa kwanza kupeana mikono.” [ Imepokewa na Abû Dâwûd, isnadi yake ni Sahîh.]