باب استحباب تشميت العاطس إِذَا حمد الله تَعَالَى وكراهة تشميته إذا لَمْ يحمد الله تَعَالَى وبيان آداب التشميت والعطاس والتثاؤب
وعن أَبي موسى رضي الله عنه قَالَ:” كَانَ الْيَهُودُ يَتَعَاطسُونَ عْندَ رسول اللهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يَرْجُونَ أنْ يَقولَ لهْم يَرْحَمُكُم الله، فيقولُ: يَهدْيكمُ اللهُ ويُصلحُ بالكم
رواه أَبو داود، والترمذي وَقالَ حديث حسن صحيح
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
142. MLANGO WA SUNNAH YA KUMWOMBEA DUA ALIEPIGA CHAFYA AKAMHIMIDI ALLÂH, UKARAHA WA KUMWOMBEA DUA IWAPO HAKUMHIMIDI ALLÂH NA UBAINIFU WA ADABU ZA KUOMBEA DUA, KUPIGA CHAFYA NA KWENDA MWAYO
Imepokewa na Abû Mûsâ (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Mayahudi walikuwa wakijipigisha chafya mbele ya Mtume ﷺ wakitaraji awaambie: “Yarhamukumullâh (Allâh Awarehemu)”, basi (badala yake) akiwaambia: “Yahdîkumullâh wa yuslihu bâlakum (Allâh Awaongoze na Awatengeneze mawazo yenu).” [ Imepokewa na Abû Dâwûd na Tirmidhy, na amesema: Hadîth hii ni Hasan Sahîh.]