باب آداب السلام
وعن أَبي أُمامة صُديِّ بن عجلان الباهِلِي رضي الله عنه قال: قال رسول الله صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: “إنَّ أوْلىَ النِّاس باللهِ مَنْ بَدأهم بالسَّلاَم”. رواه أَبُو داود بإسنادٍ جيدٍ
ورواه الترمذي عن أَبي أُمامةَ رضي الله عنهُ قِيلَ يارسولَ الله، الرَّجُلانِ يَلْتَقيان أيُّهُمَا يَبْدأُ بالسَّلامِ، قَالَ: “أوْلاهُمَا بالله تعالى
قال الترمذي: حديث حسن
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
133. MLANGO WA ADABU ZA KUTOA SALAMU
Imepokewa Abû Umâmah, Sudayyi bin ‘Ajlân al-Bâhily (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Mtume ﷺ amesema: “Hakika aliye karibu zaidi na Allâh ni yule anayeanza kuwatolea watu salamu.” [ Imepokewa na Abû Dâwûd kwa isnadi jayyid.
Vilevile Tirmidhy ameipokea kutoka kwa Abû Umâmah (Radhi za Allah ziwe juu yake): Mtume ﷺ aliulizwa: “Watu wawili wanapokutana ni yupi atakayeanza kutoa salamu?” Akajibu: “Ni yule aliye bora zaidi kwa Allâh.” [ Imepokewa na Tirmidhy, na amesema: Hadîth hii ni Hasan.]