باب كيفية السلام
عن عِمران بن حصين رضي الله عنهما قَالَ: جاءَ رجُل إِلَى النَّبيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فَقَالَ: السَّلامُ عَلَيكُم، فَرَدَّ عَلَيْهِ ثُمَّ جَلَسَ، فَقَالَ النبيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم:“عَشْرٌ”ثُمَّ جَاءَ آخَرُ فَقَالَ: السَّلامُ عَلَيكُم وَرَحْمَةُ اللهِ، فَرَدَّ عليهِ فَجَلَسَ، فَقَالَ:“عِشْرون”، ثُمَّ جَاءَ آخَرُ فَقَالَ: السَّلامُ عَلَيكُم وَرَحْمَةُ الله وَبَرَكَاتُهّ، فَرَدَّ عليهِ فَجَلَسَ، فَقَالَ:“ثَلاَثُونَ”. رواه أَبُو داود والترمذي وقال: حديث حسن
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
132. MLANGO WA NAMNA YA KUTOA SALAMU
Imepokewa na ‘Imrân bin al-Husain (Radhi za Allah ziwe juu yao) amesimulia: “Mtu mmoja alikuja kwa Mtume ﷺ , akamwamkia: “Assalâmu ‘Alaikum.” (Mtume) akamrudishia, kisha mtu yule akaketi. Mtume ﷺ akasema: “(Amepata thawabu) kumi.” Kisha akaja mtu mwingine, akasema: “Assalâmu ‘Alaikum warahmatullâhi.” Naye akamrudishia, yule mtu akaketi. Mtume ﷺ akasema: “(Amepata thawabu) ishirini.” Kisha akaja mtu mwingine, akasema: “Assalâmu ‘Alaikum warahmatullâhi wabarakâtuh.” Naye akamrudishia, yule mtu akaketi. Mtume ﷺ akasema: “(Amepata thawabu) thalathini.” [ Imepokewa na Abû Dâwûd na Tirmidhy, na amesema: Hadîth hii ni Hasan.]