0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

850. Riyadhu Swalihina Mlango Wa fadhila ya kutoa Salamu na amri ya kuisambaza

 باب فضل السلام والأمر بإفشائه


وعن الطُّفَيْل بن أُبَيِّ بن كعبٍ أنَّه كَانَ يأتي عبد الله بن عمر فيغدو مَعَهُ إِلَى السُّوقِ, قَالَ: فإذَا غَدَوْنَا إِلَى السُّوقِ, لَمْ يَمُرَّ عَبدُ الله عَلَى سَقَّاطٍ وَلاَ صَاحِبِ بيعَة وَلا مْسكين وَلا أحَدٍ إِلاَّ سَلّم عَليه، قَالَ الطُّفيلُ: فَجِئْتُ عبد الله بنَ عُمرَ يَوْماً فاستَْتَبعني إِلَى السُّوقِ فقُلْت لَهُ: ماتَصْنعُ بالسوقٍ وأنْتَ لا تَقِفُ عَلى البَيْع وَلا تَسْألُ عَن السِّلَعِ وَلا تَسُومُ بِهَا وَلا تَجلسُ في مَجَالِسِ السُّوقِ؟ وأقولُ اجْلسْ بِنَا ههُنا نَتَحدَّث، فَقَالَ يَا أَبَا بُطْن. وَكانَ الُطُّفَيلُ ذَا بَطْن إنَّما نَغُدو منْ أجْل السَّلام فنُسَلِّمُ عَلَى مَنْ لَقِيناهُ،    رواه مالك في الموُطَّإ بإسناد صحيح


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



131. MLANGO: FADHILA YA KUTOA SALAMU NA AMRI YA KUISAMBAZA


Imepokewa na AtTufail bin Ubayyi bin Ka’b ameeleza kuwa yeye alikuwa akimwendea ‘Abdullâh bin ‘Umar, akienda sokoni pamoja naye. (Akaeleza): “Tukawa tunapoenda sokoni, ‘Abdullâh akawa hapiti kwa mchuuzi wala kwa muuzaji (bidhaa za thamani kubwa) wala kwa masikini wala kwa yeyote yule ila humtolea salamu. Siku moja nikamwendea ‘Abdullâh bin ‘Umar, akanitaka nimfwate sokoni. Nikamwuliza: “Ukafanye nini sokoni nawe husimami kwa mwuzaji wala huulizii bidhaa wala hujadiliani katika bei wala huketi katika mabaraza ya sokoni?” Na nikimwambia: “Keti pamoja nasi hapa tuzungumze.” Akaniambia: “Ee Abû Batni – atTufail alikuwa ana kitambi -: “Hakika sisi tunaenda kwa ajili ya kutoa salamu, huwa tukimsalimia tunaekutana naye.”   [ Mâlik ameitaja katika kitabu chake al-Muwatta kwa isnadi Sahîh.]


Begin typing your search above and press return to search.