باب فضل السلام والأمر بإفشائه
وعن أبي هريرة رضي الله عنه عن النَّبيّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال “لما خَلَقَ الله تعالى آدَمَ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قَالَ: اذْهَبْ فَسَلِّمْ عَلَى أُولئِكَ نَفَرٍ مِنَ الَمَلاَئكة جُلُوسٌ فاسْتمعْ مايُحَيُّونَكَ فَإنَّها تَحيَّتُكَ وَتَحِيَّةُ ذُرِّيَّتِك. فَقَالَ: السَّلام عَلَيْكُمْ، فقالوا: السَّلام ُ عَلَيْكَ وَرَحْمةُ اللهِ، فَزادُوهُ: وَرَحْمةُ اللهِ” متفقٌ عَلَيْهِ.
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
131. MLANGO: FADHILA YA KUTOA SALAMU NA AMRI YA KUISAMBAZA
Imepokewa na Abû Huraira (Radhi za Allah ziwe juu yake) amehadithia: “Mtume ﷺ amesema: “Allâh Alipomwumba Adam ﷺ , Alimwambia: “Nenda ukawasalimie wale – kundi la Malaika walioketi – na usikilize watakavyokuamkia; hayo yatakuwa ndio maamkizi yako na maamkizi ya vizazi vyako.” (Adam) akaenda akawaamkia: “Assalâmu ‘Alaikum. [Amani iwe juu yenu].” Nao wakamwambia: “Assalâmu ‘Alaika warahmatullâh. [Amani iwe juu yako na Rehma za Allâh].”
Wakamzidishia: “Warahmatullâh.” [ Wameafikiana Bukhârî na Muslim.]