باب في آداب المجلس والجليس
وعن أَبي بَرْزَةَ رضي الله عنه قال: كان رسول صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقولُ بأَخَرَةٍ إذَا أرَادَ أنْ يَقُومَ مِنَ الْمَجِلسِ “سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ وبَحَمْدكَ أشْهدُ أنْ لا إلهَ إِلاَّ أنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وأتُوبُ إِلَيْكَ”فقال رَجُلٌ يارسول الله إنَّكَ لَتَقُولُ قَوْلاَ مَاكُنْتَ تَقُولُهُ فِيَما مَضَى؟ قَالَ:“ذلكَ كفَّارَةٌ لِماَ يَكُونُ في الْمجْلِسِ ” رواه أَبُو داود
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
129. MLANGO WA NIDHAMU ZA MAJILISI NA ANAYEKETI
Imepokewa na Abû Barzah (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Mtume ﷺ mwisho-mwisho wa uhai wake alikuwa akisema – anapotaka kuinuka katika majilisi: “Subhânakallâhumma wabihamdik, ash-hadu allâ-ilâha illâ anta astaghfiruka wa atûbu ilayk. [Kutakasika ni Kwako Ewe Mola wetu, na himdi zote ni Zako, nashuhudia kuwa hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki ila ni Wewe tu, nakuomba msamaha na natubia Kwako].” Mtu mmoja akamwuliza: “Yâ Rasûlallâh, hakika wewe wasema neno ambalo ulikuwa hulisemi katika siku zilizopita?” Akamjibu: “Hiyo ni kafara ya yanayopitika katika majilisi.” [ Imepokewa na Abû Dâwûd na al-Hâkim ameipokea kutoka kwa riwaya ya ‘Âisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) na akasema: isnadi yake ni Sahîh.]