0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

787. Riyadhu Swalihina Mlango Wa  Sunna Ya Kuvaa Nguo Nyeupe Na Kujuzu Kuvaa Nguo Nyekundu Kijani Manjano Na Nyeusi Na Inajuzu Nguo Ya Pamba,Kitani….

باب استحباب الثوب الأبيض، وجواز الأحمر والأخضر والأصفر والأسود، وجوازه من قطن وكتان وشعر وصوف وغيرها إِلاَّ الحرير


– وعن المغيرة بن شُعْبَةَ – رضي الله عنه -، قَالَ: كُنْتُ مَعَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – ذاتَ لَيْلَةٍ في مسير، فَقَالَ لي: { أمَعَكَ مَاءٌ؟} قلتُ: نَعَمْ، فَنَزَلَ عَنْ رَاحِلَتِهِ فَمَشَى حَتَّى تَوَارَى في سَوَادِ اللَّيْلِ، ثُمَّ جَاءَ فَأفْرَغْتُ عَلَيْهِ مِنَ الإدَاوَةِ، فَغَسَلَ وَجْهَهُ وَعَلَيْهِ جُبَّةٌ مِنْ صُوفٍ، فَلَمْ يَسْتَطِعْ أنْ يُخْرِجَ ذِرَاعَيْهِ مِنْهَا حَتَّى أخْرَجَهُمَا مِنْ أسْفَلِ الْجُبَّةِ، فَغَسَلَ ذِرَاعَيْهِ وَمَسَحَ بِرَأسِهِ، ثُمَّ أهْوَيْتُ لأَنْزَعَ خُفَّيْهِ، فَقَالَ: { دَعْهُمَا فَإنِّي أَدْخَلْتُهُمَا طَاهِرَتَيْنِ} وَمَسحَ عَلَيْهِمَا.      متفقٌ عَلَيْهِ


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Al-Mughîrah bin Shu’bah (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Usiku mmoja nilikuwa pamoja na Mtume ﷺ safarini. Akaniuliza: “Unayo maji?” Nikamjibu: “Ndio.” Akateremka kutoka katika ngamia wake, akatembea mpaka akapotea katika giza la usiku, kisha akarudi nikamminia maji kutoka katika kiriba, akaosha uso wake na alikuwa amevaa juba la sufi, basi hakuweza kuzitoa dhiraa zake katika mikono ya juba, akazitoa kwa chini ya juba, akaosha dhiraa zake na akapangusa kichwa chake. Nikainama ili nizitoe khuffu zake, akaniambia: “Ziache. Hakika nimeingiza miguu yangu ilihali ina udhu.” Akapangusa juu yake.”   [ Wameafikiana Bukari na Muslim ] 

Riwaya nyingine imesema: “..na alikuwa amevaa juba la Shamu lenye mikono membamba.”

Riwaya nyingine tena imesema: “…kisa hiki kilikuwa katika Vita vya Tabûk.”


Begin typing your search above and press return to search.