باب أدب الشرب واستحباب التنفس ثلاثاً خارج الإناء وكراهة التَّنَفُّس في الإناء واستحباب إدارة الإناء عَلَى الأيمن فالأيمن بعد المبتدئ
وعن أنس – رضي الله عنه -: أنَّ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – أُتِيَ بِلَبَنٍ قَدْ شِيبَ بماءٍ، وَعَنْ يَمِينهِ أعْرَابيٌّ، وَعَنْ يَسَارِهِ أَبُو بَكْر – رضي الله عنه -، فَشَرِبَ، ثُمَّ أعْطَى الأعْرابيَّ، وقال: { الأيْمَنَ فالأيْمَنَ} متفق عَلَيْهِ
قَوْله: { شِيب} أيْ: خُلِطَ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa na Anas (Radhi za Allah ziwe juu yao) amesimulia kuwa Mtume ﷺ aliletewa maziwa yaliochanganywa na maji, kuliani mwake alikuweko mbedui na kushotoni mwake alikuweko Abûbakar (Radhi za Allah ziwe juu yao) Akanywa kisha akampa yule mbedui, na akasema: “Kwanza hutangulizwa aliye upande wa kulia, kisha aliye upande wa kuliani mwake (yule wa pili, hadi mwisho).” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim.]