باب الحلم والأناة والرفق
قَالَ الله تَعَالَى: ﴿وَالكَاظِمِينَ الغَيْظَ وَالعَافِينَ عَنِ النَّاسِ وَاللهُ يُحِبُّ المُحْسِنينَ﴾ [ آل عمران: 134 ]
وقال تَعَالَى: ﴿خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بِالعُرْفِ وَأعْرِضْ عَنِ الجَاهِلينَ﴾ [ الأعراف: 199 ]
وقال تَعَالَى: ﴿وَلاَ تَسْتَوِي الْحَسَنَةُ وَلاَ السَّيِّئَةُ ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أحْسَنُ فَإذَا الَّذِي بَيْنَكَ وَبَيْنَهُ عَدَاوَةٌ كَأنَّهُ وَلِيٌّ حَمِيمٌ وَمَا يُلَقَّاهَا إِلاَّ الَّذِينَ صَبَرُوا وَمَا يُلَقَّاهَا إِلاَّ ذُو حَظٍّ عَظِيمٍ﴾ [ فصلت: 34-35 ]
وقال تَعَالَى: ﴿وَلَمنْ صَبَرَ وَغَفَرَ إنَّ ذَلِكَ لَمِنْ عَزْمِ الأُمُورِ﴾ [ الشورى: 43 ]
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
74. MLANGO WA KUSAMEHE NA KUWAEPUKA MAJAHILI.
Mwenyezi Mungu Amesema: “Na wanaojizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu, na Allâh Huwapenda wafanyao mema.” [3:134].
Mwenyezi Mungu Amesema: “Shikamana na kusamehe, na amrisha mema, na jitenge na majahili.” [7:199].
Mwenyezi Mungu Amesema: “Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu. Lakini hawapewi wema huu ila wanaosubiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa.” [41:34, 35].
Mwenyezi Mungu Amesema: “Na anayesubiri, na akasamehe, hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa.” [42:43].