باب التسمية في أوله والحمد في آخره
وعن حُذَيْفَةَ – رضي الله عنه -، قَالَ: كُنَّا إِذَا حَضَرْنَا مَعَ رَسُولِ اللهِ – صلى الله عليه وسلم – طَعَاماً، لَمْ نَضَعْ أيدِينَا حَتَّى يَبْدَأَ رَسُولُ الله – صلى الله عليه وسلم – فَيَضَعَ يَدَهُ، وَإنَّا حَضَرْنَا مَعَهُ مَرَّةً طَعَاماً، فَجَاءتْ جَارِيَةٌ كَأنَّهَا تُدْفَعُ، فَذَهَبَتْ لِتَضَعَ يَدَهَا في الطَّعَامِ، فَأَخَذَ رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم – بِيَدِهَا، ثُمَّ جَاءَ أَعْرَابِيّ كأنَّمَا يُدْفَعُ، فَأخَذَ بِيَدهِ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ – صلى الله عليه وسلم -: {إنَّ الشَّيْطَانَ يَسْتَحِلُّ الطَّعَامَ أنْ لا يُذْكَرَ اسمُ اللهِ تَعَالَى عَلَيْهِ، وَإنَّهُ جَاءَ بهذِهِ الجارية لِيَسْتَحِلَّ بِهَا، فأَخَذْتُ بِيَدِهَا، فَجَاءَ بهذا الأعرَابيّ لِيَسْتَحِلَّ بِهِ، فَأخذْتُ بِيَدِهِ، والَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، إنَّ يَدَهُ في يَدِي مَعَ يَدَيْهِمَا} ثُمَّ ذَكَرَ اسْمَ اللهِ تَعَالَى وَأكَلَ. رواه مسلم.
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa na Hudhaifa (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Tulikuwa tunapohudhuria pamoja na Mtume (ﷺ) katika chakula, hatuingizi mikono yetu (kuanza kula) mpaka Mtume (ﷺ) aingize mkono wake. Siku moja tulihudhuria katika chakula pamoja naye, akaja mjakazi kana kwamba anasukumwa, akataka kuingiza mkono wake katika chakula. Mtume (ﷺ) akaushika mkono wake. Kisha akaja mbedui kana kwamba anasukumwa, (Mtume (ﷺ) ) akaushika mkono wake na akasema: “Hakika shetani huhalalisha chakula kisipotajwa Jina la Allâh juu yake, naye alimleta mjakazi huyu ili akihalalishe kupitia kwake, nikaushika mkono wake, na akamleta mbedui huyu ili akihalalishe kupitia kwake, nami nikaushika mkono wake. Naapa Kwa Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake, hakika mkono wake (shetani) nimeushika kwa mkono wangu pamoja na mikono ya hawa wawili.” Kisha akataja Jina la Allâh na akala.” [ Imepokewa na Muslim.]