باب استحباب تقديم اليمين في كل مَا هو من باب التكريم
وعن أنس – رضي الله عنه -: أنَّ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – أتى مِنىً، فَأتَى الْجَمْرَةَ فَرَمَاهَا، ثُمَّ أتَى مَنْزِلَهُ بِمِنَىً ونحر، ثُمَّ قَالَ لِلحَلاَّقِ: {خُذْ} وأشَارَ إِلَى جَانِبهِ الأَيْمَنِ، ثُمَّ الأَيْسَرِ، ثُمَّ جَعَلَ يُعْطِيهِ النَّاسَ. متفقٌ عَلَيْهِ
وفي رواية: لما رمَى الجَمْرَةَ، وَنَحَرَ نُسُكَهُ وَحَلَقَ، نَاوَلَ الحَلاَّقَ شِقَّهُ الأَيْمَنَ فَحَلَقَهُ، ثُمَّ دَعَا أَبَا طَلْحَةَ الأنْصَارِيَّ – رضي الله عنه -، فَأعْطَاهُ إيَّاهُ، ثُمَّ نَاوَلَهُ الشِّقَّ الأَيْسَرَ، فَقَالَ: {احْلِقْ}، فَحَلَقَهُ فَأعْطَاهُ أَبَا طَلْحَةَ، فَقَالَ: {اقْسِمْهُ بَيْنَ النَّاسِ}
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa na Anas (Radhi za Allah ziwe juu yake) amehadithia: “Mtume (ﷺ) alienda Minâ, akaenda katika Jamratul‘aqabah, akarusha vijiwe, kisha akaenda nyumbani mwake Minâ, akachinja kisha akamwambia kinyozi: “Chukua (kichwa ukinyoe),” akaashiria upande wake wa kulia, kisha wa kushoto, halafu akawa akiwapa watu (nywele zake).” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim ]
Riwaya nyingine imesema: “Aliporusha vijiwe Jamratul‘aqabah, akamchinja dhabihu wake na akanyoa, alimpa kinyozi upande wake wa kulia, akamnyoa, kisha akamwita Abû Talha al-Ansâry (Radhi za Allah ziwe juu yake), akampa (nywele hizo), kisha akampa kinyozi upande wake wa kushoto, akamwambia: “Nyoa,” akamnyoa, akampa Abû Talha na akamwambia: “Wagawanyie watu.”