باب وداع الصاحب ووصيته عند فراقه للسفر وغيره والدعاء لَهُ وطلب الدعاء مِنْهُ
وعن عمرَ بن الخطاب – رضي الله عنه -، قَالَ: اسْتأذَنْتُ النَّبيَّ – صلى الله عليه وسلم – في العُمْرَةِ، فَأذِنَ، وقال: {لاَ تَنْسَانَا يَا أُخَيَّ مِنْ دُعَائِكَ} فقالَ كَلِمَةً ما يَسُرُّنِي أنَّ لِي بِهَا الدُّنْيَا
وفي رواية قَالَ: {أشْرِكْنَا يَا أُخَيَّ في دُعَائِكَ} رواه أَبُو داود والترمذي، وقال: {حديث حسن صحيح}
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa na ‘Umar bin al-Khattâb (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Nilimwomba Mtume (ﷺ) idhini ya kwenda ‘Umra, akaniruhusu, na akaniambia: “Ee ndugu yangu, usitusahau katika dua zako.” Neno hilo limenifurahisha mno kuliko hata kumiliki dunia yote.’
Riwaya nyingine imesema: “Ee ndugu yangu, tushirikishe nasi katika dua zako.” [ Imepokewa na Abû Dâwûd na Tirmidhy, na amesema: Hadîth hii ni Hasan Sahîh.]