باب وداع الصاحب ووصيته عند فراقه للسفر وغيره والدعاء لَهُ وطلب الدعاء مِنْهُ
وعن أَبي سليمان مالِك بن الحُوَيْرِثِ – رضي الله عنه -، قَالَ: أَتَيْنَا رسولَ الله – صلى الله عليه وسلم -، وَنَحْنُ شَبَبَةٌ مُتَقَارِبُونَ، فَأقَمْنَا عِنْدَهُ عِشْرِينَ لَيْلَةً، وَكَانَ رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم – رَحِيماً رَفيقاً، فَظَنَّ أنّا قد اشْتَقْنَا أهْلَنَا، فَسَألَنَا عَمَّنْ تَرَكْنَا مِنْ أهْلِنَا، فَأخْبَرْنَاهُ، فَقَالَ: {ارْجِعُوا إِلَى أهْلِيكُمْ، فَأقِيمُوا فِيهمْ، وَعَلِّمُوهُم وَمُرُوهُمْ، وَصَلُّوا صَلاَةَ كَذَا فِي حِيْنِ كَذَا، وَصَلُّوا كَذَا في حِيْنِ كَذَا، فَإذَا حَضَرَتِ الصَّلاَةُ فَلْيُؤَذِّنْ لَكُمْ أحَدُكُمْ وَلْيَؤُمَّكُمْ أكْبَرُكُمْ} متفقٌ عَلَيْهِ
زاد البخاري في رواية لَهُ: {وَصَلُّوا كَمَا رَأيْتُمُونِي أُصَلِّي}
وَقَوْلُه: {رحِيماً رَفِيقاً} رُوِيَ بِفاءٍ وقافٍ، وَرُوِيَ بقافينِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa na Abu Sulaimân, Mâlik bin al-Huwairith (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Tulimwendea Mtume (ﷺ) nasi tulikuwa barobaro tuliokaribiana kwa umri. Tukaketi kwake masiku ishirini. Mtume (ﷺ) alikuwa ni rahimu mwenye huruma. Akadhani kuwa tumewatamani jamaa zetu. Akatuuliza familia tulizoziacha, tukamweleza. Akatwambia: “Rudini kwa jamaa zenu, mukae kwao, muwafundishe na muwaamuru, muswali Swala kadha wakati kadha na muswali kadha wakati kadha. Wakati wa Swala ukifika, mmoja wenu awaadhinie na mkubwa wenu awaswalishe.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim].
Bukhârî ameongeza katika riwaya yake nyingine: “..na mswali kama mlivyoniona nikiswali.”
‘Umar bin al-Khattâb (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Nilimwomba Mtume (ﷺ) idhini ya kwenda ‘Umra, akaniruhusu, na akaniambia: “Ee ndugu yangu, usitusahau katika dua zako.” Neno hilo limenifurahisha mno kuliko hata kumiliki dunia yote.’
Riwaya nyingine imesema: “Ee ndugu yangu, tushirikishe nasi katika dua zako.” [ Imepokewa na Abû Dâwûd na Tirmidhy, na amesema: Hadîth hii ni Hasan Sahîh. ]