باب وداع الصاحب ووصيته عند فراقه للسفر وغيره والدعاء لَهُ وطلب الدعاء مِنْهُ
حديث زيد بن أرقم – رضي الله عنه – – الَّذِي سبق في بَابِ إكرام أهْلِ بَيْتِ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – – قَالَ: قَامَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – فِينَا خَطِيباً، فَحَمِدَ الله، وَأثْنَى عَلَيْهِ، وَوَعَظَ وَذَكَّرَ، ثُمَّ قَالَ: {أمَّا بَعْدُ، ألاَ أيُّهَا النَّاسُ، إنَّمَا أنَا بَشَرٌ يُوشِكُ أنْ يَأتِيَ رَسُولُ رَبِّي فَأُجِيبَ، وَأنَا تَارِكٌ فِيكُمْ ثَقَلَيْنِ، أوَّلَهُمَا: كِتَابُ اللهِ، فِيهِ الْهُدَى وَالنُّورُ، فَخُذُوا بِكِتَابِ اللهِ وَاسْتَمْسِكُوا بِهِ}، فَحَثَّ عَلَى كِتَابِ اللهِ، وَرَغَّبَ فِيهِ، ثُمَّ قَالَ: {وَأَهْلُ بَيْتِي، أذَكِّرُكُمُ اللهَ في أهْلِ بَيْتِي} رواه مسلم، وَقَدْ سَبَقَ بِطُولِهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa na Zaid bin Arqam (Radhi za Allah ziwe juu yake) iliotangulia katika Mlango wa Kuwakirimu Watu wa Nyumba ya Mtume (ﷺ) , akaeleza:
“Siku moja Mtume (ﷺ) alituhutubia; akamhimidi Allâh, akamsifu, akatoa waadhi, akakumbusha kisha akasema: “Ama baada ya haya. Fahamuni enyi watu! Hakika mimi ni mwanadamu, Mjumbe wa Mola wangu anakaribia kunijia nami niitike mwito wake, nami nimewaachia vizito viwili; cha kwanza ni Kitabu cha Allâh, ndani yake muna uongofu na nuru, chukueni Kitabu cha Allâh na mshikamane nacho.” Akasisitiza mno juu ya kushikamana na Kitabu cha Allâh. Kisha akasema: “Na watu wa nyumba yangu. Nawakumbusha Allâh katika watu wa nyumba yangu.” [ Imepokewa na Muslim. Imetangulia kwa urefu. [Tazama Hadîth ya 346].