باب استحباب التبشير والتهنئة بالخير
وعن ابن شِمَاسَة، قَالَ: حَضَرْنَا عَمْرَو بنَ العَاصِ – رضي الله عنه – وَهُوَ في سِيَاقَةِ الْمَوْتِ، فَبَكَى طَوِيلاً، وَحَوَّلَ وَجْهَهُ إِلَى الجِدَارِ، فَجَعَلَ ابْنُهُ، يَقُولُ: يَا أبَتَاهُ، أمَا بَشَّرَكَ رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم – بكَذَا؟ أمَا بَشَّرَكَ رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم – بِكَذَا؟ فَأقْبَلَ بِوَجْهِهِ، فَقَالَ: إنَّ أفْضَلَ مَا نُعِدُّ شَهَادَةُ أنْ لا إلهَ إِلاَّ الله، وَأنَّ مُحَمَّداً رسول اللهِ، إنِّي قَدْ كُنْتُ عَلَى أطْبَاقٍ ثَلاَثٍ: لَقَدْ رَأيْتُنِي وَمَا أحَدٌ أشَدُّ بُغضاً لرسولِ الله – صلى الله عليه وسلم – مِنِّي، وَلاَ أحَبَّ إليَّ مِنْ أنْ أكُونَ قدِ اسْتَمكنتُ مِنْهُ فَقَتَلْتُه، فَلَوْ مُتُّ عَلَى تلكَ الحَالِ لَكُنْتُ مِنْ أهْلِ النَّارِ، فَلَمَّا جَعَلَ اللهُ الإسلامَ في قَلْبِي أتَيْتُ النبيَّ – صلى الله عليه وسلم -، فقُلْتُ: ابسُطْ يَمِينَكَ فَلأُبَايِعُك، فَبَسَطَ يَمِينَهُ فَقَبَضْتُ يَدِي، فَقَالَ: {مَا لَكَ يَا عَمْرُو؟} قلتُ: أردتُ أنْ أشْتَرِطَ، قَالَ: {تَشْتَرِط مَاذا؟} قُلْتُ: أنْ يُغْفَرَ لِي، قَالَ: {أمَا عَلِمْتَ أن الإسلامَ يَهْدِمُ مَا كَانَ قَبْلَهُ، وَأن الهِجْرَةَ تَهْدِمُ مَا كَانَ قَبلَهَا، وَأنَّ الحَجَّ يَهْدِمُ مَا كَانَ قَبْلَهُ؟} وَمَا كَانَ أحدٌ أحَبَّ إليَّ مِنْ رَسُولِ الله – صلى الله عليه وسلم -، وَلاَ أجَلَّ في عَيني مِنْهُ وَمَا كُنْتُ أُطيقُ أن أملأ عَيني مِنْهُ؛ إجلالاً لَهُ، ولو سئلت أن أصفه مَا أطقت، لأني لَمْ أكن أملأ عيني مِنْهُ، ولو مُتُّ عَلَى تِلْكَ الحالِ لَرجَوْتُ أن أكُونَ مِنْ أهْلِ الجَنَّةِ، ثُمَّ وَلِينَا أشْيَاءَ مَا أدْرِي مَا حَالِي فِيهَا؟ فَإذَا أنَا مُتُّ فَلاَ تَصحَبَنِّي نَائِحَةٌ وَلاَ نَارٌ، فَإذا دَفَنْتُمُونِي، فَشُنُّوا عَليَّ التُّرابَ شَنّاً، ثُمَّ أقِيمُوا حَوْلَ قَبْرِي قَدْرَ مَا تُنْحَرُ جَزورٌ، وَيُقْسَمُ لَحْمُهَا، حَتَّى أَسْتَأنِسَ بِكُمْ، وَأنْظُرَ مَا أُرَاجعُ بِهِ رسُلَ رَبّي. رواه مسلم
قَوْله: {شُنُّوا} رُوِي بالشّين المعجمة والمهملةِ، أيْ: صُبُّوه قَليلاً قَليلاً، والله سبحانه أعلم
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa na Ibnu Shumâsah amesimulia: “Tulimtembelea Amru bin al-‘Âs (Radhi za Allah ziwe juu yake) naye amefikwa na mauti, akalia kitambo kirefu na akaugeuza uso wake ukutani. Mwanawe akawa anamwambia: “Ee baba yangu! Kwani Mtume (ﷺ) hakukubashiria jambo kadhaa? Mtume (ﷺ) hakukubashiria jambo kadhaa?” Akaelekea kwa uso wake, akasema: “Hakika kitu bora kabisa tulichokiandaa ni kushahadia Lâ-ilâha illallâh, Muhammadur-rasûlullâh [Hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allâh, na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allâh]. Mimi nilikuwa katika hali tatu: (1) Nilikuwa nikijiona kuwa hakuna yeyote anayemchukia zaidi Mtume (ﷺ) kuniliko, na nilipendelea mno lau kama ningalimakinika nikamwuua. Basi lau ningalikufa katika hali hiyo, ningalikuwa mtu wa motoni. Allâh Aliponijaalia Uislamu moyoni mwangu, nilimwendea Mtume (ﷺ) nikamwambia: “Nyosha mkono wako nikubai.” Akaunyosha mkono wake nami nikaukunja mkono wangu, akaniuliza: “Unani ee ‘Amru?” Nikamwambia: “Nataka nitoe sharti.” Akaniuliza: “Utoe sharti ya jambo gani?” Nikamwambia: “Nisamehewe.” Akaniambia: “Kwani hujui kwamba Uislamu huvunja yalio kabla yake, Hijra huvunja yalio kabla yake na Hajj huvunja yalio kabla yake?” (2) Hakuna yeyote niliekuwa nikimpenda mno kama Mtume (ﷺ) , wala hakuna aliyekuwa mtukufu machoni mwangu kama yeye, nilikuwa siwezi kumtaamali kwa sababu ya kumtukuza. Lau ningaliulizwa nitoe wasifu wake, nisingaliweza, kwa sababu nilikuwa siwezi kumtaamali. Lau ningalikufa katika hali hiyo, nataraji ningalikuwa mtu wa Peponi. (3) Kisha tukaja kuyasimamia mambo, ambapo sijui hali yangu itakuwaje! Basi nitakapokufa, nisifuatwe na mwombolezaji wala moto. Mtakaponizika, mtanifukia polepole kwa mchanga, halafu mtaketi kando ya kaburi langu kitambo cha kuchinjwa ngamia na kugawanywa nyama yake ili nipumbazike nanyi na nitazame nitakalowajibu Wajumbe wa Mola wangu.” [ Imepokewa na Muslim.]