بابُ حفظ السِّر
وعن عائشة – رضي الله عنها -، قالت: كُنَّ أزْوَاجُ النَّبيِّ – صلى الله عليه وسلم – عِنْدَهُ، فَأقْبَلَتْ فَاطِمَةُ – رضي الله عنها – تَمْشِي، مَا تُخْطِئُ مِشيتُها مِنْ مشْيَةِ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – شَيْئاً، فَلَمَّا رَآهَا رَحَّبَ بِهَا، وقال: {مَرْحَباً بابْنَتِي}، ثُمَّ أجْلَسَهَا عَنْ يَمِينِهِ أَوْ عَنْ شِمَالِهِ، ثُمَّ سَارَّهَا فَبَكتْ بُكَاءً شَديداً، فَلَمَّا رَأى جَزَعَهَا، سَارَّهَا الثَّانِيَةَ فَضَحِكَتْ، فقلتُ لَهَا: خَصَّكِ رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم – مِنْ بَيْنِ نِسَائِهِ بالسِّرَارِ، ثُمَّ أنْتِ تَبْكِينَ ! فَلَمَّا قَامَ رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم – سَألْتُهَا: مَا قَالَ لَكِ رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم -؟ قالت: مَا كُنْتُ لأُفْشِي عَلَى رسول الله – صلى الله عليه وسلم – سِرَّهُ، فَلَمَّا تُوُفِّيَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – قُلْتُ: عَزَمْتُ عَلَيْكِ بِمَا لِي عَلَيْكِ مِنَ الحَقِّ، لَمَا حَدَّثْتِنِي مَا قَالَ لَكِ رسول الله – صلى الله عليه وسلم -؟ فقالتْ: أمَّا الآن فَنَعَمْ، أمَّا حِيْنَ سَارَّنِي في المَرَّةِ الأُولَى فأخْبَرَنِي أنّ جِبْريلَ كَانَ يُعَارِضُهُ القُرآنَ في كُلِّ سَنَةٍ مَرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ، وَأنَّهُ عَارَضَهُ الآنَ مَرَّتَيْنِ، وَإنِّي لا أُرَى الأجَلَ إِلاَّ قَدِ اقْتَرَبَ، فَاتَّقِي اللهَ وَاصْبِرِي، فَإنَّهُ نِعْمَ السَّلَفُ أنَا لَكِ، فَبَكَيْتُ بُكَائِي الَّذِي رَأيْتِ، فَلَمَّا رَأى جَزَعِي سَارَّنِي الثَّانِيَةَ، فَقَالَ: {يَا فَاطِمَةُ، أمَا تَرْضَيْنَ أنْ تَكُونِي سَيِّدَةَ نِسَاءِ المُؤُمِنِينَ، أَوْ سَيَّدَةَ نِساءِ هذِهِ الأُمَّةِ؟} فَضَحِكتُ ضَحِكِي الَّذِي رَأيْتِ. متفقٌ عَلَيْهِ،
وهذا لفظ مسلم
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Âisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Wakeze Mtume (ﷺ) walikuwa kwake. Akaja Fâtima (Radhi za Allah ziwe juu yake) akitembea, mwendo wake hautofautiani hata kidogo na mwendo wa Mtume (ﷺ). (Mtume) alipomuona alimkaribisha kwa kusema: “Karibu binti yangu!” Akamketisha kuliani mwake au kushotoni mwake. Kisha akazungumza naye kwa siri, Fâtima akalia sana. (Mtume) alipomuona amefazaika, akamzungumzia kwa siri mara ya pili, akacheka. Nikamwuliza: “Mtume (ﷺ) amekuhusisha peke yako kwa siri bila ya kuwashirikisha wakeze kisha wewe unalia?” Mtume (ﷺ) alipoondoka, nilimwuliza: “Mtume (ﷺ) alikwambia nini?” Akajibu: “Siwezi kuitoa siri ya Mtume (ﷺ).” Mtume (ﷺ) alipoondoka duniani, nikamwambia: “Nakuapia kwa haki nilionayo kwako, hukuniambia alilokwambia Mtume (ﷺ) (sasa niambie).” Akasema: “Ama sasa nitakuzungumzia. Ama aliponinong’onezea kwa mara ya kwanza, aliniambia kuwa Jibrîl alikuwa akimsomea Qur’âni mara moja au mbili kila mwaka, mara hii amemsomea mara mbili, (akasema:) “Nami naona mauti yamekaribia, basi mche Allâh na usubiri, kwani mimi ndiye mtangulizi bora kwako.” Ndipo nikalia kilio ulichokiona. Aliponiona nimefazaika, akaninong’onezea mara ya pili, akaniambia: “Ee Fâtima, ama huridhiki uwe ndiye Nana wa wanawake wa Waumini?,” au alisema: “Nana wa wanawake wa umati huu?” Nikacheka kicheko ulichokiona.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim] . Hadîth hii ni kwa lafdhi ya Muslim.