0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

67. MLANGO WA UKARAHA WA KUTAMANI MAUTI KWA SABABU YA KUPATWA NA MADHARA, WALA HAPANA UBAYA (KUYATAMANI) KWA KUCHELEA FITNA KATIKA DINI

بابُ كراهة تمنّي الموت بسبب ضُرّ نزل بِهِ وَلاَ بأس بِهِ لخوف الفتنة في الدين


عن أَبي هريرة – رضي الله عنه -: أنَّ رسول الله – صلى الله عليه وسلم -، قَالَ: { لا يَتَمَنَّ أحَدُكُمُ المَوْتَ، إمَّا مُحْسِناً فَلَعَلَّهُ يَزْدَادُ، وَإمَّا مُسِيئاً فَلَعَلَّهُ يَسْتَعْتِبُ}      متفقٌ عَلَيْهِ، وهذا لفظ البخاري

وفي رواية لمسلم عن أَبي هريرة – رضي الله عنه -، عن رسول الله – صلى الله عليه وسلم -، قَالَ: { لاَ يَتَمَنَّ أَحَدُكُمُ المَوْتَ، وَلاَ يَدْعُ بِهِ مِنْ قَبْلِ أنْ يَأتِيَهُ؛ إنَّهُ إِذَا مَاتَ انْقَطَعَ عَمَلُهُ، وَإنَّهُ لاَ يَزِيدُ المُؤْمِنَ عُمُرُهُ إِلاَّ خَيْراً}


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



67. MLANGO WA UKARAHA WA KUTAMANI MAUTI KWA SABABU YA KUPATWA NA MADHARA, WALA HAPANA UBAYA (KUYATAMANI) KWA KUCHELEA MATATIZO KATIKA DINI


Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Mtume amesema: “Asitamani mauti mmoja wenu. Ima atakuwa ni mtenda mema, huenda akazidisha, na ima ni mtenda mabaya, huenda akarudi kwa Allâh.”    [ Wameafikiana Bukhari na Muslim]
Riwaya nyingine ya Muslim iliopokewa na Abû Huraira (Radhi za Allah ziwe juu yake) kutoka kwa Mtume amesema: “Mmoja wenu asitamani mauti, wala asiyaombe kabla hayajamfikia, hakika atakapokufa matendo yake yatakatika, na hakika kila unapozidi umri wa Mwumini ndio huzidi kheri.”


Begin typing your search above and press return to search.