0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

667. Riyadhu Swalihina Mlango wa Wajibu wa Kuwatii wenye madaraka Katika Jambo Ambalo Si la Kumuasi Allah na Uharamu wa Kuwatii katika Maasia

 باب وجوب طاعة ولاة الأمر في غير معصية وتحريم طاعتهم في المعصية


 وعن عبدِ اللهِ بن عمرو – رضي الله عنهما -، قَالَ: كنا مَعَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – في سَفَرٍ، فَنَزَلْنَا مَنْزِلاً، فَمِنَّا مَنْ يُصْلِحُ خِبَاءهُ، وَمِنّا مَنْ يَنْتَضِلُ، وَمِنَّا مَنْ هُوَ في جَشَرِهِ، إذْ نَادَى مُنَادِي رسولِ الله – صلى الله عليه وسلم -: الصَّلاةَ جَامِعَةً . فَاجْتَمَعْنَا إِلَى رسولِ الله – صلى الله عليه وسلم -، فَقَالَ: { إنَّهُ لَمْ يَكُنْ نَبيٌّ قَبْلِي إِلاَّ كَانَ حَقّاً عَلَيْهِ أنْ يَدُلَّ أُمَّتَهُ عَلَى خَيْرِ مَا يَعْلَمُهُ لَهُمْ، وَيُنْذِرَهُم شَرَّ مَا يَعْلَمُهُ لَهُمْ. وَإنَّ أُمَّتَكُمْ هذِهِ جُعِلَ عَافِيَتُهَا في أوَّلِهَا، وَسَيُصيبُ آخِرَهَا بَلاَءٌ وَأمُورٌ تُنْكِرُونَهَا، وَتَجِيءُ فِتنَةٌ يُرَقِّقُ بَعْضُهَا بَعْضاً، وَتَجِيءُ الفتنَةُ فَيقُولُ المُؤْمِنُ: هذه مُهلكتي، ثُمَّ تنكشفُ، وتجيء الفتنةُ فيقولُ المؤمنُ: هذِهِ هذِهِ. فَمَنْ أحَبَّ أنْ يُزَحْزَحَ عَنِ النَّارِ، ويُدْخَلَ الجَنَّةَ، فَلْتَأتِهِ منيَّتُهُ وَهُوَ يُؤْمِنَ باللهِ واليَوْمِ الآخِرِ، وَلْيَأتِ إِلَى النَّاسِ الَّذِي يُحِبُّ أنْ يُؤتَى إِلَيْهِ. وَمَنْ بَايَعَ إمَاماً فَأعْطَاهُ صَفْقَةَ يَدِهِ، وَثَمَرَةَ قَلْبِهِ، فَلْيُطِعْهُ إن استَطَاعَ، فإنْ جَاءَ آخَرُ يُنَازِعُهُ فَاضْرِبُوا عُنْقَ الآخَرِ}      رواه مسلم


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa ‘Abdullâh bin  ‘Amri (Radhi za Allah ziwe juu yake ) amesimulia: “Tulikuwa na Mtume (ﷺ) katika safari fulani. Tukateremka mahala, miongoni mwetu muna waliokuwa wakitengeneza hema lao, muna waliokuwa wakishindana kurusha mishale na muna waliokuwa wakiwaangalia wanyama wao. Mara mtangazaji wa Mtume (ﷺ) akanadi: “Hudhurieni muswali pamoja.” Tukajumuika kwa Mtume (ﷺ) , akatwambia: “Hakika kila Nabii aliekuja kabla yangu ilikuwa ni haki juu yake awajulishe umati wake kheri anayoijua kwao na awaonye shari anayoijua kwao. Hakika umati wenu huu, umejaaliwa usalama wake ni mwanzoni mwake. Hakika mwisho wa umati huu utafikiwa na balaa na mambo mtakayoyachukia, zitakuja fitina (majaribu na mitihani) ambazo baadhi yake zitalainisha nyingine (zitakazokuja zitakuwa kubwa kuliko zilizopita). Fitna itakuja, Mwumini atasema: “Hapa ndio maangamivu yangu,” kisha itaondoka. Itakuja fitna nyingine, Mwumini atasema: “Hii ndio kubwa zaidi.” Basi anayependa aepushwe na moto na aingizwe Peponi, afanye hima mauti yake yamfikie ilihali anamwamini Allâh na Siku ya mwisho, awatendee watu analopenda kutendewa. Na atakayembai kiongozi akampa kifungo cha baia yake na tunda la moyo wake, amtii akiweza; atapokuja mwingine akijitakia utawala, basi mkateni shingo yake.”     [Imepokewa na Muslim.]

Begin typing your search above and press return to search.