باب وجوب طاعة ولاة الأمر في غير معصية وتحريم طاعتهم في المعصية
وعن ابن عمر – رضي الله عنهما، قَالَ: سَمِعْتُ رسول الله – صلى الله عليه وسلم -، يقول: { مَنْ خَلَعَ يَداً مِنْ طَاعَةٍ لَقِيَ اللهَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلاَ حُجَّةَ لَهُ، وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ في عُنُقِهِ بَيْعَةٌ، مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً} رواه مسلم
وفي رواية لَهُ: { وَمَنْ مَاتَ وَهُوَ مُفَارِقٌ لِلجَمَاعَةِ، فَإنَّهُ يَمُوتُ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً}
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa ‘Abdullâh bin ‘Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake ) amesema: “Nimemsikia Mtume (ﷺ) akisema: “Atakayetoka katika utiifu (wa kiongozi), atakutana na Allâh wala hatakuwa na hoja ya kumtetea. Na atakayekufa ilihali shingoni mwake hana baia (hakubai), atakuwa amekufa kifo cha kijahiliya.” [ Imepokewa na Muslim.]
Riwaya yake nyingine imesema: “..na atakayekufa naye amefarikiana na jamaa (umoja wa Waislamu), hakika atakufa kifo cha kijahiliya.”