0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

651. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Kuwa Na Ghadhabu Yanapokeukwa Matakatifu Ya Allah Na Kuinusuru Dini Yake

باب الغضب إِذَا انتهكت حرمات الشّرع والانتصار لدين الله تعالى


وعن أنس – رضي الله عنه -: أنَّ النبيَّ – صلى الله عليه وسلم – رَأى نُخَامَةً في القبلَةِ، فَشَقَّ ذَلِكَ عَلَيْهِ حَتَّى رُؤِيَ في وَجْهِهِ؛ فَقَامَ فَحَكَّهُ بِيَدِهِ، فَقَالَ: { إن أحدَكُمْ إِذَا قَامَ فِي صَلاَتِهِ فَإنَّهُ يُنَاجِي رَبَّهُ، وَإنَّ رَبَّهُ بَيْنَهُ وَبيْنَ القِبلْةِ، فَلاَ يَبْزُقَنَّ أحَدُكُمْ قِبَلَ الْقِبْلَةِ، وَلَكِنْ عَنْ يَسَارِهِ، أَوْ تَحْتَ قَدَمِهِ} ثُمَّ أخَذَ طَرَفَ رِدَائِهِ فَبَصَقَ فِيهِ، ثُمَّ رَدَّ بَعْضَهُ عَلَى بَعْضٍ، فَقَالَ: { أَوْ يَفْعَلُ هكذا}     متفقٌ عَلَيْهِ

وَالأمرُ بالبُصَاقِ عَنْ يَسَارِهِ أَوْ تَحْتَ قَدَمِهِ هُوَ فِيما إِذَا كَانَ في غَيْرِ المسجِدِ، فَأمَّا في المسجدِ فَلاَ يَبصُقُ إِلاَّ في ثَوْبِهِ


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Mtume (ﷺ) aliona kohozi (Msikitini) upande wa Qibla, jambo hilo likawa zito kwake hata ikaonekana (ghadhabu) usoni mwake. Akainuka na akalisugua kwa mkono wake, akasema: “Kwa hakika mmoja wenu anaposimama katika Swala yake hakika anazungumza na Mola wake, na hakika Mola wake Yuko baina yake na Qibla. Basi mmoja wenu asiteme katu mate upande wa Qibla, lakini ateme kushotoni mwake au chini ya mguu wake.” Kisha akachukua ncha ya shuka yake, akatema humo halafu akairudisha baadhi yake juu ya baadhi nyingine. Akasema: “Au afanye hivi.”     [ Wameafikiana Bukhari na Muslim].   


Begin typing your search above and press return to search.